Kadi za mialiko
Mandhari
Kadi za mialiko ni barua au kadi ziandikwazo kwa dhumuni la kumwalika mtu ahudhurie sherehe au kikao fulani.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa kadi za mialiko ni:
- 1, jina la mwandishi na anwani yake.
- 2, jina la mwandikiwa.
- 3, lengo la mwalikaji kwa ufupi.
- 4, tarehe ya mwaliko.
- 5, mahali pa kukutana.
- 6, wakati wa kukutana.
- 7, jibu lipelekwe kwa nani.
Mfano wa kadi ya mwaliko ni hii: Bw. na bi. Kiiza Karugaba wa Bukoba Karagwe wanayo furaha kuwaalika Bw. na Bi., Dr., Mch., Prof. Kelvin Radius kwenye sherehe ya arusi yao itakayofanyika tarehe 17-01-2018 kwenye kanisa la Mt. Josephine Bakhita, Nanenane, saa tisa alasiri, na baadaye nyumbani kwao Bukoba Karagwe saa mbili usiku. Jibu kwa Felix Macheo, S.L.P. 30675 Bukoba.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kadi za mialiko kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |