Nenda kwa yaliyomo

Jumuiya ya Wanavyuoni Waislamu wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Logo yake.

Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika (pia: Umoja wa Maulama Afrika; kwa Kifaransa: Union des Ulemas d'Afrique)[1]

Ni chombo huru cha Kiislamu kinacholenga kuunganisha maulama wa bara la Afrika kusini kwa Sahara[2].

Umoja huo ulianzishwa mwaka 2011 BK mjini Bamako.

Makao makuu yako katika jiji la Bamako nchini Mali.

Alama ya Umoja wa wanazuoni ni ramani ya bara la Afrika yenye rangi ya kijani kibichi pamoja na alama ya mnara wa msikiti.[3]

Tovuti ilionyesha kwenye Septemba 2020 majina ya wanachama 531, kati yao 29 kutoka Kenya, 14 kutoka Komori, 15 kutoka Tanzania na 7 kutoka Uganda[4].

Katika mwaka 2020 umoja huo ulitoa tamko kuhusu mlipuko wa Covid-19 ambako ulikubali hatua dhidi ya ugonjwa huu pamoja na kufunga misikiti kwa muda.[5]

  1. Tovuti ya umoja huo unatumia maumbo tofautitofauti ya jina lake kwa Kiswahili na Kiingereza, tena mara nyingi kwa tahajia yenye makosa.
  2. http://africanulama.org/sw/taswira-ya-utambulisho/ Utambulisho kwenye tovuti ya Umoja
  3. Taarifa ya Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Ulema Dkt. Said Bourhani Abdallah pembeni mwa mkutano mkuu wa pili wa umoja huo huko Mecca 2018 wakati wa mkutano na wanahabari juu ya kuunda Muungano
  4. http://africanulama.org/sw/wanachama-wa-umoja/ Wanachama wa Umoja, iliangaliwa Septemba 2020
  5. http://africanulama.org/fr/2020/03/23/position-de-lunion-des-ulemas-dafrique-a-propos-de-la-pandemie-coronavirus-covid-19/ Archived 13 Agosti 2020 at the Wayback Machine. Position de l'union des ulemas d'Afrique a propos de la pandemie coronavirus (Covid-19), iliangaliwa Septemba 2019