Nenda kwa yaliyomo

Julia Salzano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Julia.

Julia Salzano (Santa Maria Capua Vetere, Caserta, 13 Oktoba 1846Casoria, Napoli, 17 Mei 1929) alikuwa sista wa Kanisa Katoliki nchini Italia na mwanzilishi wa shirika la Masista wa Katekesi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu (21 Novemba 1905) kwa ajili ya kufundisha imani na maadili ya Kikristo na kueneza ibada kwa ekaristi takatifu[1].

Kabla ya kuwa mtawa, Julia Salzano alikuwa mwalimu na kuanzia mwaka 1865 alifanya kazi Casoria alipojitokeza kama katekista bora pia.[2][3]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Aprili 2003, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91400
  2. "Saint Giulia Salzano". Saints SQPN. 13 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Saint Giulia Salzano". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.