Joseph Fourier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Joseph Fourier
Kaburi la Fourier mjini Paris

Jean Baptiste Joseph Fourier (21 Machi 1768 - 16 Mei 1830) alikuwa mtaalamu wa hisabati na fizikia kutoka nchini Ufaransa.

Alionekana kuwa na vipaji vikubwa alipokuwa mwanafunzi shuleni mjini Auxerre. Alipofikia umri wa miaka 18 alipewa kazi ya profesa palepale. 1705 alihamia Paris akawa profesa ya hisabati.

Pamoja na Napoleoni alikwenda Misri mwaka 1799 akashiriki katika utafiti wa nchi. Baada ya kurdi alikuwa mkuu wa mkoa wa Isère baadaye wa mkoa wa Rhone.

Tangu 1815 aliishi mjini Paris akawa Katibu wa akademia ya sayansi.

Pamoja na shughuli hizi zote alifanya utafiti mbalimbali za kifizikia. Alieleza jinsi gani joto linapanua ndani ya gimba mango na hii huitwa Kanuni za Fourier.

Alibuni pia mbinu kadhaa za hisabati zilizo muhimu kwa fizikia ya kisasa.