John Fisher

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. John Fisher.

John Fisher au John wa Rochester (146922 Juni 1535) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kule Uingereza.

Pamoja na Thomas More, alimkataa mfalme Henry VIII aliyejitenga na Kanisa Katoliki la Roma. Kwa hiyo, John Fisher alifungwa na baada ya kushtakiwa mahakamani aliuawa kwa kukatwa kichwa. Hapo katikati Papa Paulo III alimteua kuwa kardinali.

Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Desemba 1886, halafu Papa Pius XI alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 19 Mei 1935.

Sikukuu yake inadhimishwa pamoja na ile ya Thomas More tarehe 22 Juni katika Kanisa Katoliki[1], na 6 Julai katika Kanisa Anglikana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Orodha yake inapatikana katika Joseph Gillow's Bibliographical Dictionary of the English Catholics (London, s.d.), II, 262–270. Kati ya vitabu vyake 26, muhimu zaidi ni:

 • Treatise concernynge...the seven penytencyall Psalms" (London, 1508);
 • Sermon...agayn ye pernicyous doctrin of Martin Luther (London, 1521);
 • Defensio Henrici VIII" (Cologne, 1525);
 • De Veritate Corporis et Sanguinis Christi in Eucharistia, adversus Johannem Oecolampadium (Cologne, 1527);
 • The Ballad of Barry Buttock, a Cautionary Tale (London, 1529);
 • De Causa Matrimonii...Henrici VIII cum Catharina Aragonensi (Alcalá de Henares, 1530);
 • The Wayes to Perfect Religion (London, 1535);
 • A Spirituall Consolation written...to hys sister Elizabeth (London, 1735).

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • E. Surtz, "The Works and Days of John Fisher," Boston: Harvard University Press, 1967.
 • E.E. Reynolds, "Saint John Fisher," Wheathampstead: Anthony Clarke, 1972.
 • "Humanism, Reform and the Reformation: The Career of Bishop John Fisher," edited by B. Bradshaw & Eamon Duffy, Cambridge University Press, 1989.
 • Richard Rex, "The Theology of John Fisher," Cambridge University Press
 • "The English Works of John Fisher, Bishop of Rochester (1469–1535): Sermons and other Writings, 1520–1535," edited by Cecilia A. Hatt, Oxford University Press, 2002.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.