Jiminyano wa Modena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Jiminyano, alivyochorwa na Simone Martini, Fitzwilliam Museum, Cambridge.

Jiminyano wa Modena (Cognento, Modena, Emilia-Romagna, Italia, 15 Januari 312 - Modena, 31 Januari 397) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 342/344 ingawa kwanza alikimbia jukumu hilo alipochaguliwa akiwa bado shemasi tu[1].

Alimaliza Upagani jimboni na kupambana na Uario ulioenea sana huko akishirikiana na Ambrosi wa Milano.

Pia alipata umaarufu kwa kufukuza pepo hata akaitwa Konstantinopoli akaponye binti kaisari.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Januari[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/39175
  2. Martyrologium Romanum, 2004
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.