Janvière Ndirahisha
Tarehe ya kuzaliwa | 1966 |
Mahali pa kuzaliwa | Burundi |
Kazi | Mwanasiasa |
Janvière Ndirahisha (kuzaliwa Burundi, 1966) ni msomi na mwanasiasa. Kutoka mwaka 2015 mpaka 2020 alikuwa waziri wa elimu nchini Burundi. Ni rais wa National Women's Forum (FNF).
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Janvière Ndirahisha aliyapata masomo yake kutoka Chuo Kikuu cha Burundi akaendelea kupata shahada ya uzamili kutoka University of Antwerp. Tasnifu yake kuhusu Grothiendiek representations ilisimamiwa na Fred Van Oystaeyen.[1]
Ndirahisha alichaguliwa kuwa Rais wa kongamano jipya la kimataifa la wanawake Burundi katika mwaka wa 2013.[2]
Katika mwaka wa 2015, Agosti, Ndirahisha alitangazwa kama Waziri wa Elimu, Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi katika baraza la mawaziri la Pierre Nkurunziza [3] Kufikia mwaka wa 2019 alikuwa ameshakuwa Waziri wa Elimu, Ufundi na Mafunzo ya Ufundi naye Gaspard Banyankimbona akiwa Waziri wa Elimu, Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi [4]
Katika mwaka wa 2017, Ndirahisha alitangaza kuwa walimu wakuu wa shule ambazo zilikuwa zimepata chini ya asilimia thelathini, 30% katika mitihani ya kitaifa wangeachishwa kazi na wizara yake ikafunga shule kadhaa zilizofeli. [5] Katika mwaka wa 2018 wizara yake ikapiga marufuku wasichana wajawazito kutoka kuhudhuria shule, hatua ambayo ilikosolewa na wapigania haki sawa nchini.[6]
Mrithi wa Rais Nkurunziza Évariste Ndayishimiye aliondoa Ndirahisha kutoka baraza la mawaziri mnamo mwaka wa 2020.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Scott W. Williams. "Janviere Ndirahisha". Black Women in Mathematics. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.
- ↑ Diane Uwimana (26 Mei 2014). "Women's forum: a slow step". IWACU English News. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Government of Burundi". Embassy of the Republic of Burundi in Ankara. 24 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Burundi". The Economist Intelligence Unit. 1 Mei 2019. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Diane Uwimana. "Six "unauthorized" basic schools to be closed in Bujumbura". Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nita Bhalla. "Burundi school ban on expectant teens 'skewed' against girls' education", 4 July 2018.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Janvière Ndirahisha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |