Évariste Ndayishimiye
Evariste Ndayishimiye (amezaliwa 1968) ni askari mwanasiasa ambaye amekuwa Rais wa Burundi tarehe 18 Juni2020[1] baada ya kifo cha Pierre Nkurunziza tarehe 8 Juni 2020.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa katika familia ya Wahutu nchini Burundi. Wakati wa kuanzishwa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Burundi alikuwa mwanafunzi wa sheria kwenye chuo kikuu cha Burundi. Baada ya mashambulio dhidi ya wanafunzi Wahutu alijiunga na chama cha CNDD–FDD akaendelea kuwa kiongozi wa tawi lake la wanamgambo. Baada ya mapatano ya kumaliza vita alikuwa makamu wa mkuu wa jeshi la kitaifa.
Baada ya uchaguzi wa kiongozi wa CNDD-FDD Pierre Nkurunziza kuwa rais, Ndayishimiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani hadi mwaka 2007 na baadaye mwangalizi wa jeshi lote hadi 2014[2].
Mwaka 2016 alikuwa katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD. Nkurunziza alipokubali kutogombea tena urais alimkubali Ndayishimiye kuwa mgombea wa chama kama rais[3].
Katika uchaguzi wa mwaka 2020 Ndayishimiye alishinda kwa kupata asilimia 68 za kura zote. Nkurunziza aliaga dunia ghafla tarehe 8 Juni 2020 mara baada ya uchaguzi. Mahakama Kuu ya Burundi ilikubali kuwahishwa kwa kuapishwa kwa rais mpya na tarehe 18 Juni Ndayishimiye alikula kiapo cha kuhudumia kama rais wa taifa[4].
Anaishi katika ndoa na Angeline Ndayubaha.[5] Anajulikana kama Mkristo mwaminifu wa Kanisa Katoliki.[6]
Mnamo Agosti 2024, ripoti ya Amnesty International ilishutumu vitendo vya "vitisho, unyanyasaji, ukamataji ovyo na kuwekwa kizuizini" vinavyofanywa na serikali ya Évariste Ndayishimiye kwa kulenga wanaharakati, waandishi wa habari na wengineo.[7].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Le président Ndayishimiye prend tête de Burundi fragilisé. la-croix.com ya 18 Juni 2020
- ↑ "Evariste Ndayishimiye candidat du pouvoir au scrutin de mai au Burundi", Deutsche Welle, 27 January 2020. Retrieved on 11 June 2020.
- ↑ "Burundi's ruling party names presidential hopeful", BBC News, 2020-01-26. Retrieved on 2020-05-07. (en-GB)
- ↑ Burundi swears in Evariste Ndayishimiye as president, tovuti ya Africa News ya 18-06-2020
- ↑ [1]
- ↑ Qui est le général Evariste Ndayishimiye, le nouveau visage du régime burundais ? , tovuti ya rtbf.be, redio ya Ubelgiji
- ↑ [https://www.rfi.fr/fr/afrique/20240821-burundi-le-pr%C3%A9sident-ndayishimiye-continue-de-mener-une-implacable-r%C3%A9pression-pointe-amnesty Afrique Burundi: le président Ndayishimiye continue de mener une «implacable répression», pointe Amnesty], tovuti ya Radio France International ya 21-08-2024
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Évariste Ndayishimiye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |