Hoteli ya Queen Elizabeth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hoteli ya Queen Elizabeth
Ilianzishwa 1958
Mmiliki Hoteli za Fairmont
Aina ya kampuni Hoteli
Vyumba: 1039
Vyumba vya aina ya suiti: 100
Mikahawa: 4
Magorofa : 21
Makao Makuu ya kampuni Montreal, Quebec, Kanada
Tovuti http://www.fairmont.com/queenelizabeth

Hoteli Le Reine Élizabeth[1] au Queen Elizabeth (jina rasmi la Kifaransa ni Fairmont Le Reine Élizabeth, jina rasmi la Kiingereza ni Fairmont The Queen Elizabeth) ni hoteli kubwa iliyo jijini Montreal, Quebec.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ujenzi ulikamilika mwaka 1958 chini ya Shirika la reli la Kanada (Canadian National Railway) lakini likauzwa hapo baadaye kwa kampuni ya Hoteli za Canadian Pacific, hivi sasa Hoteli za Fairmont.

Hoteli hii ilikuwa na vyumba 1039 na magorofa 21 na kuifanya iwe hoteli kubwa kabisa karika Mkoa wa Quebec, Kanada na hoteli ya pili kubwa nchini Kanada ya Hoteli za Fairmont. Hoteli kubwa kabisa ya Fairmont nchini Kanada ni Royal York jijini Toronto, ambayo ina vyumba 1365.

Inapatikana katika anwani ya 900 Boulevard René Lévesque Ouest, katikati mwa Montreal, na hivyo basi imeshikamana na stesheni ya treni.

Wageni wengi mashuhuri walikaa huko, wakiwa ni pamoja na Malkia Elizabeth II (mara nne) na Duke wa Edinburgh, Malkia Mama, Prince Charles, Fidel Castro, ambaye alikuwa mkuu wa nchi wa kwanza kutembelea hoteli hiyo, Charles de Gaulle, na Princess Grace wa Monako, wakati wa Expo '67, Indira Gandhi, Jacques Chirac, Nelson Mandela, Dalai Lama, Mikhail Gorbachev, Jimmy Carter, Henry Kissinger, Perry Como, Joan Crawford, John Travolta, na Mikhail Baryshnikov.

Hoteli hii ilipata umaarufu dunia nzima wakati John Lennon na Yoko Ono, walikuwa wamekatazwa kuingia Marekani walipolala huko wakarekodi wimbo wao Give Peace a Chance katika chumba cha 1742 cha hoteli hiyo, hapo kati ya 26 Mei na 2 Juni 1969.

Tamasha la Orodha ya Wachezaji waliochaguliwa na NHL liliandaliwa mara 10 katika hoteli hiyo kati ya miaka 1963 na 1979.

Katika mwaka wa 1970, serikali ya Quebec ilihamisha kituo cha operesheni zake ikawa ndani ya hoteli hii wakati wa shida za Oktoba wa mwaka huo.

Watu wachache hukumbuka utata uliozuka katika kulipa hoteli hiyo jina. Wapenzi wa Quebec walitaka iitwe Château Maisonneuve kwa makumbusho ya mwanzilishi wa Montreal, Paul Chomedey de Maisonneuve. Rais wa CN,Donald Gordon alisisitiza kuwa iitwe jina la malkia ,ambaye alikuwa amepanda na kuchukua kiti cha utawala kwa ghafla bila kutarajiwa. Alipokuwa anakuwa malkia,hoteli hiyo ilikuwa ikichorwa na wataalamu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Jina la Kifaransa, Le Reine Elizabeth, inaweza kusumbua mtu akili kwa sababu ya matumizi ya neno la kuashiria wanaume le. Maelezo yake ni kuwa neno hilo halitumiki hapo kwa ajili ya nomino Reine bali ni kwa nomino Hôtel.