Nenda kwa yaliyomo

Indira Gandhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Indira Gandhi pamoja na rais wa Marekani Richard Nixon 1971

Indira Gandhi (19 Novemba 191731 Oktoba 1984) alikuwa mwanasiasa wa Uhindi na mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.

Indira alizaliwa kama binti wa Jawaharlal Nehru aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uhindi kati ya 1947 hadi 1964. Jina la Gandhi alipokea kwa njia ya ndoa na Firuz Gandhi ambaye hakuwa na uhusiano na Mahatma Gandhi.

Alishirikiana na babake kama karani yake. Mwaka 1955 alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha Congress. Baada ya kifo chake aliingia katika serikali kama waziri akachaguliwa kuwa waziri mkuu 1966 akatawala hadi 1977.

1980 alirudi baada ya uchaguzi akashika uongozi tena. Kipindi cha mwisho kiliona uasi wa kundi la Kalasinga huko Punjab. Indira iliamuru jeshi kuvamia Hekalu ya Kalasinga huko Amritsar ambako waasi wenye silaha walijificha. Baada ya tendo hili Indira aliuawa na walinzi wake waliokuwa Kalasinga.

Baada ya kifo chake, madaraka yalishikiliwa na mtoto wake wa kiume aitwae Rajiv Gandhi, na alikuwa kama waziri mkuu kati ya 1984 hadi 1989.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Indira Gandhi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.