Hongwe
Hongwe | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Hongwe mweupe (Galeichthys feliceps)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 30:
|
Hongwe, fumi au yahudhi ni samaki wa baharini na maji baridi katika familia Ariidae wa oda Siluriformes ambao wana sharubu ndefu. Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki duniani kote. Familia hii ina spishi 143.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Hongwe wana pezimkia lenye panda ndefu. Kwa kawaida jozi tatu za sharubu zipo. Wana magamba ya ufupa juu ya kichwa chao na karibu na pezimgongo lao. Angalau spishi kadhaa zina miiba yenye sumu katika pezimgongo na mapeziubavu.
Msambazo na makazi
[hariri | hariri chanzo]Hongwe sio wa kawaida kati ya samaki kama kambale kwa kuwa huishi hasa katika bahari; nyingi sana za familia za samaki kama kambale huishi katika maji baridi tu na wana uvumilivu mdogo kwa hali ya maji ya chumvi. Hongwe hupatikana katika bahari yenye kina kidogo za kitropiki karibu na pwani za Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, Afrika, Asia na Australia.
Hata hivyo, spishi nyingi kiasi za hongwe zimo pia katika makazi ya maji baridi au hutokea katika maji baridi tu. Huko Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, karibu na spishi 43 huingia maji ya chumvi kidogo au hupatikana katika maji baridi pekee. Na hata katika Afrika spishi kadhaa zinatokea maji baridi hasa.
Ekolojia
[hariri | hariri chanzo]Liche ya makazi yao ya kibahari hongwe wana matohoaji kadhaa ya kipekee ambayo yanawaweka tofauti na samaki wengine kama kambale. Takriban spishi zote ni samaki wanaoatamia mayai kinywani. Madume hubeba idadi ya makumi machache ya mayai madogo kinywani kwa muda wa miezi miwili hadi wachanga watoke na kuanza kuogelea peke yao.
Uvuvi
[hariri | hariri chanzo]Hongwe huvuliwa sehemu nyingi za Afrika, hata Afrika ya Mashariki. Kwa kawaida huliwa wakiwa wamechomwa au katika supu ya samaki.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Arius africanus, Hongwe Mashariki (African sea catfish)
- Arius brunellii, Hongwe wa Mto Juba (Jubba River catfish)
- Arius festinus, Hongwe Mwepesi (Agile catfish)
- Arius gigas, Hongwe Mkubwa Magharibi (Giant sea catfish)
- Arius latiscutatus, Hongwe Kichwa-shupavu (Rough-head sea catfish)
- Arius madagascariensis, Hongwe wa Madagaska (Madagascar sea catfish)
- Arius uncinatus, Hongwe Ndaka (Barbed catfish)
- Arius venosus, Hongwe Mapezi-meusi (Veined catfish)
- Carlarius heudelotii, Hongwe Domo-laini (Smoothmouth sea catfish)
- Carlarius parkii, Hongwe wa Gini (Guinean sea catfish)
- Galeichthys ater, Hongwe Mweusi (Black sea catfish)
- Galeichthys feliceps, Hongwe Mweupe (White sea catfish)
- Galeichthys trowi, Hongwe wa Trow (Trow's sea catfish)
- Netuma thalassina, Hongwe Mkubwa Mashariki (Giant catfish)
- Plicofollis dussumieri, Hongwe Mapezi-nchanyeusi (Blacktip sea catfish)
- Plicofollis layardi, Hongwe Miiba-myembamba (Thinspine sea catfish)
- Plicofollis polystaphylodon, Hongwe wa Msumbiji (Mozambique sea catfish)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Hongwe mkubwa mashariki
-
Hongwe mapezi-nchanyeusi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hongwe kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 9 Desemba 2019 kwenye Wayback Machine.