Homo neanderthalensis
Mandhari
Homo neanderthalensis | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Sanamu ya mwanamume katika makumbusho
| ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
|
Homo neanderthalensis alikuwa kiumbehai wa jamii ya binadamu (Hominidae). Pengine spishi hii inachukuliwa kama nususpishi (kwa jina la Homo sapiens neanderthalensis). Utafiti wa DNA umeonyesha walifanana na binadamu wa leo kwa asilimia 99.7.
Walienea katika Mashariki ya Kati, Ulaya Magharibi na kusini hadi Asia ya Kati.
Kabla hawajatoweka miaka 40,000 iliyopita, waliweza kuzaliana na Homo sapiens baada ya huyo kutoka nje ya Afrika na hivi kurithisha sehemu ya jeni zao kwa binadamu wasio wa Kusini kwa Sahara.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Homo neanderthalensis kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |