Nenda kwa yaliyomo

Hekaya ya Genji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji kwa mlango wa 20 – 朝顔 Asagao na Tosa Mitsuoki (1617–1691).

Hekaya ya Genji (kwa Kijapani 源氏物語 Genji Monogatari) ni kati ya riwaya za kwanza za fasihi ya Japani.[1]

Hadithi hii ya mwanamfalme Genji inasomwa na kuheshimiwa hadi leo katika utamaduni wa Japani.

Iliandikwa na mwandishi wa kike Murasaki Shikibu mnamo mwanzo wa karne ya 11 BK.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Genji ni mwana wa mfalme Kiritsubo wa Japani na hawara (mke wa kando) anayependwa na baba yake lakini mfalme hawezi kumpa nafasi juu ya mrithi wake rasmi. Kufuatana na mila anapewa jina tofauti ya familia Minamoto (aka Genji), hahitaji kufanya kazi, lakini anapewa mafunzo katika usanii na michezo ya kijeshi.

Akiwa na umri mdogo anaanza kutamani wanawake na ilhali ana cheo cha juu anaweza kutimiza tamaa zake. Anaanza mapenzi na wanawake wengi wa aina mbalimbali.

Baada ya kujiuzulu kwa mfalme mzee kuna matatizo na mfalme mpya na mama yake aliyetelekezwa baada ya mama yake Genji. Genji anaondoka kwa hiari yake katika ikulu ya kifalme lakini baadaye anaweza kurudi.

Wakati wa kukaa nje anamzaa mtoto wake wa kwanza lakini hawezi kurudi kwenye ikulu pamoja na mpenzi wake Murasaki.

Anaendelea kufanya mapenzi na wanawake wengi, anashindwa kuwa mwaminifu kwa mmoja, akikaa na wanawake mbalimbali katika nyumba yake.

Baada ya kifo cha mpenzi wake, Genji hana nguvu ya kuishi tena. Riwaya haielezi jinsi gani anavyoaga dunia.

Sehemu ya mwisho wa riwaya inasimulia habari za wanawe Niou na Kaoru lakini pia hadithi hii inakwisha kwa ghafla.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nussbaum, Louis-Frédéric. (2002). "Genji-monogatari" in Japan Encyclopedia, p. 237.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]