Nenda kwa yaliyomo

Grato wa Oloron

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake katika kanisa la kijiji alipozaliwa.

Grato wa Oloron (pia: Grat, Gratus; Lichos, leo nchini Ufaransa, karne ya 5 - Jaca, baada ya 506) alikuwa askofu wa kwanza wa Oloron wakati wa mfalme Alariki II wa Wagoti kutawala Akwitania.

Alishiriki Mtaguso wa Agde[1] ambao uliongozwa na Sesari wa Arles na kukusudia kurekebisha hali ya Kanisa katika eneo hilo [2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Oktoba[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.