Grace Gao (mwanaharakati)
Grace Gao (anajulikana pia kama Grace Geng[1]; amezaliwa 1993) ni mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Uchina. Yeye ni binti Gao Zhisheng, wakili wa Kichina wa haki za binadamu na mpinga sera za serikali.[2][3] Yeye na familia yake wamepelelezwa, kupigwa, na kutishwa na mamlaka za Uchina.[3] Anaelimisha kimataifa ili kutangaza kitabu cha baba yake A China More Just na kutilia mkazo kwenye kesi yake (kwa sasa, ametoweka na mamlaka za Uchina zinahusika na kutoweka kwake[4]), na kusema dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Uchina.[3] "Kwa hiyo, ninajikuta katika nafasi ya kuchukua vazi hilo na kuwa mtetezi wa haki za binadamu kama baba yangu... Ukweli ni nguvu na nitaendelea kuongea mpaka baba yangu awe huru".[5][6]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Gao alikuwa akisindikizwa kwenda shuleni kila siku na maafisa wa polisi ambao walimfuata kila alikoenda.[3] Grace alijijeruhiwa kwa sababu ya huzuni na maumivu[7] na, akiwa na umri wa miaka 17, alijaribu kujiua mara kadhaa.[2] Alipata ugumu kuelewa maamuzi ya baba yake.[2]
Baada ya Gao kuzuiwa na serikali kuhudhuria shule,[3] mama yake aliamua kuwasafirisha yeye pamoja na kaka yake (Peter, b. 2005) kutoka Uchina.[3] Mnamo tarehe 9 Januari 2009, walikimbilia Uthai kwa usafiri wa pikipiki na basi (wakiwa wamejificha kwenye sehemu ya kubeba mizigo),[8] kisha wakaenda Merika ambako walipewa hifadhi ya kisiasa.[8][9] Huko New York, Grace alipata matibabu hospitalini kwa miezi sita kwa maswala ya afya ya akili lakini bado ilikua ngumu kuamini watu.[2] Alijifunza kumwelewa baba yake[8] na kumsaidia.[2]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Grace alijifunza Kiingereza baada ya kuhamia Merika, alihitimu shule ya upili akiwa na miaka 20,[8] na kuendelea kusoma uchumi katika chuo kikuu cha California.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Grace Geng: Chinese dissident's daughter proud of her 'brave' father", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2016-06-14, iliwekwa mnamo 2021-09-16
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Citizen Power Initiatives for China", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-01-05, iliwekwa mnamo 2021-09-16
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 "Grace Gao | Speakers | Oslo Freedom Forum". web.archive.org. 2017-08-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-15. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
- ↑ "A year on, lawyer's disappearance highlights China's escalating human rights disaster". Hong Kong Free Press HKFP (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2018-08-13. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
- ↑ Av Hanne Mauno. "– Jeg var sjokkert. Men jeg har vokst opp i et Kina som hjernevasket meg". Dagsavisen (kwa Kinorwe). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
- ↑ Grace Geng, 'Truth is power and I will keep speaking it until my father is free'(03/10/16) for International Service for Human Rights Ilihifadhiwa 25 Juni 2021 kwenye Wayback Machine. Iliwekwa mnamo 2021-09-16
- ↑ "'My Father Never Spoke About The Persecution He Suffered'". Radio Free Asia (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
- ↑ 8.0 8.1 8.2 8.3 "A Hero's Daughter". National Review (kwa American English). 2017-06-25. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
- ↑ hermesauto (2016-06-14). "China rights lawyer Gao Zhisheng ready for consequences over new book: Daughter". The Straits Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.