Gervas Kasiga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Gervas Kasiga
AmezaliwaGervas 'Rutakirwa' Kasiga
UtaifaMTanzania
MhitimuB.A Fine and Performing Arts & M.A Kiswahili Literature
Kazi yakeMwigizaji, Mwandishi wa Miswada ya Filamu, Mwongozaji wa Filamu, Mhadhiri wa Filamu na Fasihi
Miaka ya kazi2001-hadi sasa

Gervas 'Rutakirwa' Kasiga (majina yake maarufu ni Chuma na/au Junior.[1]; alizaliwa 4 Februari 1982) ni mwigizaji wa filamu, mwandishi wa miswada ya filamu, mwongozaji wa filamu anayeheshimika nchini Tanzania.

Anafahamika sana kwa kuongoza filamu maarufu ya "Fake Pastors (2007)" na kuongoza kuchagua waigizaji wa filamu ya Bongoland II.

Ameandika miswada kadhaa ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga (Tamthilia) kama vile "Gharika" na "Dira", miswada ya filamu maarufu za Unfortunate Love, Ripple of Tears, Village Pastor, Wende na nyinginezo.

Mwaka 2011 filamu yake fupi ya Wende ilichaguliwa kuoneshwa katika Tamasha la Sita la Filamu la Kimataifa la Kenya (KIFF). Vilevile amepata kuwa balozi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) akiwakilisha wanafilamu wa ki-Tanzania.

Kasiga ameshafanya kazi mbalimbali za kisanaa na mashirika kama AMREF, PATHFINDER, THE NATURE AND CONSERVANCY, The International Theatre and Literacy Project (ITLP), CRDB - TANZANIA, College of Mathematics and Natural Science - University of Dodoma, Vocation Training Centre of Tanzania (VETA), Regina University - Canada https://www.slideshare.net/WSCSD/kasiga n.k. Ameshaendesha mafunzo mbalimbali ya uigizaji, uandishi wa miswada ya filamu, uchukuaji picha za video pamoja uongozaji katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Dodoma na Dar es salaam. Mafunzo hayo amekuwa akiyafanya aidha kupitia taasisi yake ya Dodoma Arts Center (DAC) au kupitia kampuni yake ya Bona Fide Films ama kwa kushirikiana na mashirika ya ndani na ya kimataifa.

Msanii huyu pia ni Mhadhiri wa masomo ya Fasihi na Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma - Tanzania.

Vilevile ni mwanablogu, anaendesha blogu ya Sebuleni.[2][3][4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Majina hayo aliyapata kupitia mifululizo ya vipindi maarufu vya tamthilia za kituo cha runinga cha ITV (Tanzania) kupitia kundi la Kaole Sanaa Group.
  2. Gervas Kasiga katika seti ya Bongoland II
  3. Kibira anamtambulisha Kasiga katika ushiriki wa Bongoland II 2008 - Kibira blogu.
  4. Gervas Kasiga katika blogu ya Sebuleni.