Nenda kwa yaliyomo

Galus I wa Clermont

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Galus I wa Clermont (Clermont-Ferrand, leo nchini Ufaransa, 489 hivi - Clermont-Ferrand, 553 hivi) alikuwa askofu wa 16 wa mji huo kuanzia mwaka 527 hadi kifo chake[1].

Mtoto wa makabaila, alikataa ndoa akawa mmonaki mnyenyekevu na mpole. Kwanza alifanywa padri, halafu askofu, akaongoza kwa ufanisi mkubwa[2], kama ilivyoandikwa na Gregori wa Tours, aliyekuwa mwanafunzi wake na mwana wa ndugu yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Mei[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/53140
  2. Jones, Terry. "Gall". Patron Saints Index. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-09. Iliwekwa mnamo 2007-11-09.
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.