Gaël Faye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gaël Faye

Maelezo ya awali
Amezaliwa (1982-08-06)6 Agosti 1982
Bujumbura, Burundi
Aina ya muziki Hip Hop
Kazi yake Rapa, mtunzi wa muziki, mwandishi

Gaël Faye (alizaliwa Bujumbura, Burundi, 6 Agosti 1982) ni rapa, mtunzi wa muziki, na mwandishi Mfaransa-Mnyarwanda.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Gaël Faye alizaliwa mwaka wa 1982 mjini Bujumbura nchini Burundi. Mama yake ni mrwanda na baba yake ni mfaransa. Mama yake alikwenda kuishi Ufaransa lakini Gaël Faye alikaa Burundi na baba yake. Baada ya mwanzo wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi mwaka wa 1993 na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka wa 1994, alikimbia nchi yake ya asili hadi nchini Ufarasa mwaka 1995. Alikuwa na umri wa miaka 13.[1][2] Alikua na mama yake wakati wa ujana mjini Versailles katika wilaya ya Yvelines nchini Ufaransa.[1] Alifurahishwa na muziki wa hip hop.[3]

Gaël Faye alisoma katika sekondari ya Jules-Ferry mjini Versailles, kisha katika shule ya biashara.[1][4] Halafu alipata shahada ya uzamili katika usimamizi wa fedha na alifanya kazi kwa miaka miwili katika kampuni ya kitegauchumi jijini London. Baadaye alitoka jijini kufanya uandishi na muziki.

Mwaka wa 2015, alihama na mke wake na binti zao wawili kuishi nchini Rwanda.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Gaël Faye na Edgar Sekloka waliunda bendi ya Milk Coffee and Sugar.[1] Walichapisha albamu ya kwanza mwaka wa 2009 na wameipa jina albamu hii Découverte du Printemps de Bourges mwaka wa 2011.[5]

Gaël Faye alichapisha albamu ya kwanza peke yake ambayo inaitwa Pili pili sur un croissant au beurre mwaka 2012. Albamu hii inasimulia tawasifu ya mwimbaji binafsi. Katika nyimbo Gaël Faye anahadithia kuhusu uhamisho, vita, Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, na mapenzi.[5]

Gaël Faye alitoa tarehe 19 Oktoba 2018 wimbo wa Balade brésilliene na mwimbaji mbrazil Flavia Coelho.[6]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

2013: Pili Pili sur un croissant au beurre

EP[hariri | hariri chanzo]

  • 2017: Rythmes et botanique
  • 2018: Des fleurs

Uandishi[hariri | hariri chanzo]

Mwezi Agosti mwaka 2016, kitabu chake cha kwanza ambacho kinaitwa Petit Pays (jina ambalo linamaanisha nchi ndogo) kilichapishwa na Grasset. Kitabu hiki kwa kiasi kidogo ni tawasifu na kinahusu Gabriel, mtoto Mfaransa-Mnyarrwanda ambaye ameishi katika usalama miaka ya 1990 nchini Burundi. Akiwa na umri wa miaka kumi mwaka wa 1992 nchini Burundi, lakini baada ya mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, maisha ya Gabriel yanabadilika.[7]

Kitabu kilipata tuzo nyingi mwaka wa 2016 kama Prix du roman Fnac, Prix du premier roman français, Prix Goncourt des lycéeens, na Prix du roman des étudiants France Culture-Télérama.[8] Kitabu kimeuzwa zaidi ya nakala milioni nchini Ufaransa. Filamu ya simulizi ya kitabu hiki, ambayo inaitwa Petit Pays pia, itachapishwa katika jumba la sinema mwaka wa 2020. Mwendeshaji filamu ni Éric Barbier.[7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "FAYE Gaël". www.frereolivier.fr. Iliwekwa mnamo 2020-04-12. 
  2. Grey, Tobias (2018-05-29), "A French-Rwandan Rap Star Turned Novelist From Burundi", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2020-04-12 
  3. "Gaël Faye, rappeur tout en finesse". Télérama.fr (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2020-04-12. 
  4. "Gaël Faye, l’écrivain rappeur". Yvelines Infos (kwa fr-FR). 2017-06-20. Iliwekwa mnamo 2020-04-12. 
  5. 5.0 5.1 "Gael Faye: l’homme qui pimente le rap français". Slate Afrique (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2020-04-12. 
  6. "Balade brésilienne (avec Flavia Coelho)". Le Canal Auditif (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2020-04-12. 
  7. 7.0 7.1 "Petit pays - ReMev", Gaël Faye (kwa Kifaransa). 2020-02-19. 
  8. "Gaël Faye reçoit le 4e Prix du roman des étudiants France Culture-Télérama". Livres Hebdo (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2020-04-12.