Furukombe
Mandhari
Furukombe | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki ni ndege mbuai wa nusufamilia Haliaeetinae katika familia Accipitridae.
Ndege hao ni baina ya tai wakubwa kabisa. Uzito wao unatofautiana kutoka kg 2 (furukombe wa Sanford) mpaka 9 (furukombe wa Steller).
Manyoya yao yana rangi ya kahawia mpaka nyeusi lakini kichwa, mkia, kidari na tumbo ni nyeupe kufuatana na spishi. Furukombe wa Madagaska, wa Sanford na wa Ulaya wana kichwa hudhurungi.
Spishi zote zinatokea karibu na maji ama baridi ama ya bahari. Hula samaki hasa lakini ndege wengine, mizoga na mara kwa mara wanyama wadogo pia.
Hujenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au mwamba. Jike hutaga mayai 1-3.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Haliaeetus vocifer, Furukombe wa Afrika (African Fish Eagle)
- Haliaeetus vociferoides, Furukombe wa Madagaska (Madagascar Fish Eagle)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Haliaeetus albicilla (White-tailed Eagle)
- Haliaeetus leucocephalus (Bald Eagle)
- Haliaeetus leucogaster (White-bellied Sea Eagle)
- Haliaeetus leucoryphus (Pallas's Fish Eagle)
- Haliaeetus pelagicus (Steller's Sea Eagle)
- Haliaeetus sanfordi (Sanford's Sea Eagle)
- Ichthyophaga humilis (Lesser Fish Eagle)
- Ichthyophaga ichthyaetus (Grey-headed Fish Eagle)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Furukombe wa Afrika
-
Furukombe wa Madagaska
-
White-tailed eagle
-
Bald eagle
-
White-bellied sea eagle
-
Pallas's fish eagle
-
Steller's sea eagle
-
Lesser fish eagle
-
Grey-headed fish eagle