Furukombe wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Furukombe
Furukombe baada ya kumshika samaki
Furukombe baada ya kumshika samaki
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Accipitriformes (Ndege kama vipanga)
Familia: Accipitridae (Ndege walio na mnasaba na vipanga)
Jenasi: Haliaeetus
Spishi: H. vocifer
Daudin, 1800)

Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki (Haliaeetus vocifer[1]) ni spishi mkubwa wa tai. Yeye ndiye ndege wa kitaifa wa nchi za Zimbabwe na Zambia.

Ndege anayefanana naye zaidi ni Furukombe wa Madagaska (H. vociferoides) ambaye yumo hatarini sana kuangamizwa. Kama tu tai wote wa bahari wenye aina mbili maalum, huyu ana spishi mwenye kichwa cheupe (Furukombe) na mwingine mwenye kichwa cha hudhurungi. Hawa ni ndege wa zamani sana, na kwa hivyo wao huwa na makucha, midomo, na macho ya rangi nyeusi (Wink na wengineyo, 1996). Spishi wote wawili wana angalau mikia yenye rangi nyeupe, ikiwemo hata makinda.

Sifa[hariri | hariri chanzo]

Yai la furukombe wa Afrika

Furukombe ni ndege mkubwa, na ule wa kike ana uzani wa kilo 3.2-3.6 (paundi 7-8) na ni mkubwa kuliko ule wa kiume ambaye ana uzani wa 2-2.5kg (paundi 4.4-5.5). Ndege wa kiume kawaida huwa na mabawa yenye upana wa mita 2 (futi 6), huku ndege wa kike wakiwa na mabawa yenye upana wa mita 2.4 (futi8). Urefu wao ni sentimita 63-75 (incha 25-30). Wao huweza kutofautishwa rahisi sana na ndege wengine huku miili yao ikiwa ya rangi ya kahawia, na mabawa yao meusi huwa na nguvu nyingi. Kichwa, kifua na mkia ya furukombe wote ina rangi nyeupe kama theluji na mdomo uliojipinda, ambao mara nyingi ni wa rangi ya samawati lakini ncha yake huwa nyeusi.

Wanapopatikana[hariri | hariri chanzo]

Spishi huyu mara nyingi hupatikana katika maziwa yenye maji yasiyokuwa na chumvi, mabwawa ya maji, au mito ingawa wakati mwingine wao huweza kupatikana karibu na pwani katika maeneo ambapo mito inaingia baharini. Furukombe wana asili yao Barani Afrika, huku wakipatikana katika maeneo makubwa ya Afrika ya upande kusini mbele ya ncha ya chini ya Jangwa la Sahara.

Kuzaana[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa kuzaana wa furukombe ni wakati wa msimu wa kiangazi, wakati ambapo viwango vya maji vimepungua. Furukombe huaminika kuendelea na shughuli za kuzaana maisha yao yote, na furukombe wawili mara nyingi huwa na viota viwili wanayvovitumia tena na tena. Kwa sababu viota vyao mara nyingi hutumika tena na tena na kuboreshwa kupitia kipindi cha miaka mingi, vinaweza kuwa vikubwa sana, huku vingine vikifikia mita 2 (futi sita) kwa upana na mita 1.2 (futi 4) kwa undani. Viota vyao hujengwa katika mti mkubwa na hujengwa mara nyingi kwa kutumia vijiti na vipande vingine vya mbao.

Furukombe wa kike hutaga kati ya yai 1 au 3, ambayo ni meupe na yenye madoadoa mekundu. Mayai hulaliwa na furukombe wa kike, lakini ndege wa kiume atayalalia mayai wakati ndege wa kike anapoenda kuwinda. Mayai huchukua muda wa kati ya siku 42 na 45 kuanguliwa. Mayai mara nyingi yataanguliwa siku tofauti, na makinda wa kwanza kawaida atawauwa wowote watakaozaliwa baada ya yeye. Makinda hukomaa baada ya siku 70 hadi 75, na baada ya wiki 8 makinda atakuwa tayari kujuilisha na kawaida huanza kutoka nje ya kiota baada wiki 2 baadaye.

Furukombe mara nyingi husimama mitini huku miili yao ikiwa wima vilivyo.

Lishe[hariri | hariri chanzo]

Furukombe mara nyingi hula samaki, ambao, anapowaona kutoka mtini aliposimama, anashuka chini haraka na kuwanyakua kutoka majini kwa kutumia makucha yake makubwa na kupaa juu tena kumla samaki Yule. Ikiwa furukombe atampata samaki mwenye zaidi ya uzani 1.8 (paudni 4) atakuwa mzito sana kuruhusu kupaa angani, kwa hivyo atamvuruta majini hadi afikie ufuo wa maji. Ikiwa samaki ni mzito kiasi kwamba hawezi kupaa kabisa, atamuangusha majini na kuelekea hadi ufuo ulio karibu zaidi. Pia samaki Yule hula ndege wa majini, mamba wachanga na mizoga.

Ishara[hariri | hariri chanzo]

Picha za ndege katika nembo ya Namibia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Maelezo chini ya ukurasa[hariri | hariri chanzo]

  1. Asili ya jina: Haliaeetus, kutoka Kilatini, maana "tai wa bahari"; vocifer, kutoka neno la Kilatini vox, "sauti", + -fer, kiumbe anayebeba kitu fulani, ili kuashiria kelele zinazofanywa na ndege huyu anapoita. Sauti hizi, wakati anapokaa, hutolewa huku kichwa kikiwa kimeinamishwa nyuma kabisa, jambo ambalo si la kawaida katika tai wa bahari isipokuwa katika spishi hii na ile ya Madagaska (furukombe Malagasi).
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons