Nenda kwa yaliyomo

Frediani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Frediano akielekeza mto upande wa bahari.

Frediani (pia: Frigianu; Eire ya Kaskazini[1], karne ya 6; Lucca, Italia wa leo, 18 Machi 588 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 560 hivi[2].

Kabla ya hapo alikuwa mmonaki tena mkaapweke karibu na Lucca. Waumini walikwenda kumtafuta upwekeni awe askofu wao. Alikusanya waklero waishi monasterini.

Alifaulu kuleta wavamizi Walombardi katika Kanisa Katoliki lakini pia kuchimba mfereji wa kuelekeza mto Serchio baharini ili kugeuza madimbwi kuwa mashamba[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Machi[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Online, Catholic. "St. Frediano - Saints & Angels". Catholic Online (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-09-07.
  2. "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Lucca". www.newadvent.org. Iliwekwa mnamo 2020-09-07.
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/78150
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.