Felix wa Cantalice

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Felix wa Cantalice katika kazi yake ya ombaomba alivyochorwa na Pieter Paul Rubens.

Felix wa Cantalice ndilo jina la kitawa la Felice Porri (Cantalice, Rieti, Italia, 1515 hivi - Roma 18 Mei 1587) aliyekuwa bruda wa urekebisho wa Ndugu Wadogo Wakapuchini, mwenye unyofu na ugumu wa maisha wa ajabu, ambaye kwa miaka 40 alifanya kazi ya ombaomba[1] kwa ajili ya watawa wenzake na kwa ajili ya fukara akieneza upendo na amani mjini Roma [2] [3].

Alitangazwa mwenye heri tarehe 1 Oktoba 1625 na mtakatifu tarehe 22 Mei 1712, wa kwanza wa shirika hilo kutangazwa hivyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Mei[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. ""Who is St. Felix of Cantalice?" Felician sisters International, May 17 2013". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-09. Iliwekwa mnamo 2023-03-09. 
  2. ""Saint Felix of Cantalice", Felician Sisters of North America". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-23. Iliwekwa mnamo 2023-03-09. 
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/53750
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.