Felix de Andreis
Felix de Andreis, C.M., (12 Desemba 1778 – 15 Oktoba 1820) alikuwa mkuu wa kwanza wa Shirika la Utume (Wavinsenti) nchini Marekani na Makamu Mkuu wa Louisiana ya juu huko St. Louis.[1]
Andreis alizaliwa kaskazini mwa Italia. Kazi yake ya awali ilikuwa kufundisha theolojia katika Chuo cha Propaganda huko Roma, kinachofundisha makasisi kwa ajili ya kazi ya umisionari.
Louis Dubourg alimshawishi Andreis mwaka 1815 kwenda kufanya kazi katika eneo la Missouri. Aliwasili St. Louis mwaka 1817. Akiwa amewekwa kama makamu mkuu na Dubourg, Andreis pia aliongoza miradi kadhaa ya kielimu na ya kiroho, ikiwa ni pamoja na kuwa kiongozi wa kiroho wa Rose Philippine Duchesne.[2]
Maandishi ya kiroho ya Andreis yaliidhinishwa na wanatheolojia tarehe 15 Aprili 1917, na mchakato wa kuthibitisha utakatifu wake ulifunguliwa rasmi tarehe 25 Julai 1918, ukimpatia cheo cha Mtumishi wa Mungu.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Felix de Andreis - Catholic Encyclopedia article
- ↑ Dictionary of Missouri Biography. University of Missouri Press. 1999. ku. 11–12.
- ↑ Index ac status causarum beatificationis servorum dei et canonizationis beatorum (kwa Latin). Typis polyglottis vaticanis. Januari 1953. uk. 68.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |