Msambia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Eriobotrya japonica)
Msambia (Eriobotrya japonica) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Msambia ukichanua
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Msambia au mplamu wa Japani (Eriobotrya japonica) ni kichaka kikubwa au mti mdogo wa familia Rosaceae. Matunda yake yaliyo matamu au machungu kidogo huitwa masambia. Ikiwa yameiva yana rangi ya manjano.
Asili ya mti huu ni Uchina lakini hutokea pia huko Japani, Korea na milima ya Uhindi na Pakistani. Siku hizi hupandwa duniani kote katika maeneo yasiyo na joto au baridi sana. Katika Afrika ya Mashariki huonekana sana.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Majani
-
Maua
-
Masambia mtini
-
Masambia sokoni