Elimu nchini Singapore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Singapur, Ministry of Education Language Centre


Elimu nchini Singapur inasimamiwa na Wizara ya Elimu (MOE), ambayo inasimamia maendeleo na utawala wa shule za serikali zinazopokea fedha za walipa kodi, lakini pia ina jukumu la ushauri na usimamizi juu ya shule binafsi.

Kwa shule zote, za binafsi na za serikali, kuna tofauti katika kiwango cha uhuru katika mtaala wao, wigo wa msaada wa fedha toka kwenye kodi na ufadhili.

Matumizi ya elimu mara nyingi huwa asilimia 20 ya bajeti ya kitaifa ya mwaka, ambayo inasaidia elimu ya shule za serikali na elimu ya shule za binafsi kwa wananchi wa Singapore. Wasio-raia hubeba gharama kubwa zaidi za kuelimisha watoto wao katika shule za serikali na pia za binafsi.

Mwaka wa 2000 Sheria ya Elimu ya Lazima ilifanya kuwa kosa la jinai kwa wazazi kutoandikisha shuleni watoto wa umri wa shule za msingi (ila wale walio na ulemavu), na kuhakikisha kuwa walihudhuria mara kwa mara.

Lugha kuu ya kufundishia huko Singapore ni Kiingereza, ambayo ilikuwa rasmi lugha ya kwanza ndani ya mfumo wa elimu mwaka 1987. Kiingereza ni lugha ya kwanza iliyofundishwa kwa nusu ya watoto wanapofikia umri wa shule ya chekechea na inakuwa msingi wa mafundisho wakati wanapofika shule ya msingi. Ingawa Kimalay, Mandarin na Kitamil pia ni lugha rasmi, lugha ya Kiingereza ni lugha ya mafundisho kwa karibu masomo yote isipokuwa lugha za asili na masomo ya fasihi ya lugha hizo; hizi kwa ujumla hazifundishwi kwa Kiingereza, ingawa kuna uhuru wa kutumia Kiingereza katika hatua za mwanzo.

Mfumo wa elimu ya Singapore umeelezewa kuwa mfumo bora kabisa duniani. Singapore ina kiwango kikubwa cha wanafunzi wanaofaulu duniani.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elimu nchini Singapore kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.