Edbati wa Lindisfarne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edbati wa Lindisfarne (jina asili: Eadberht; alifariki 6 Mei 698) alikuwa mmonaki, halafu askofu wa Lindisfarne kuanzia mwaka 688 hadi kifo chake.

Mwanafunzi wa Cuthbert wa Lindisfarne, alikuwa maarufu kwa ujuzi wa Biblia, utekelezaji wa amri za Mungu na hasa kwa ukarimu wake kwa maskini[1].

Hata baada ya kupewa uaskofu alitumia muda wa kutosha katika kimya na sala pamoja na kushika ufukara.

Tangu kale anaadhimishwa na Wakatoliki[2] na Waorthodoksi[3] kama mtakatifu, hasa tarehe aliyofariki dunia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Fryde, E. B.; Greenway, D. E.; Porter, S.; Roy, I. (1996). Handbook of British Chronology (toleo la Third revised). Cambridge, UK: Cambridge University Press. ISBN 0-521-56350-X.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.