Ebitoke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ebitoke ni mchekeshaji anayechekesha watu kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram n.k. Yeye ni Mkerewe ila amezaliwa kijiji cha Kiuwani, wilaya ya Muleba Vijijini, mkoa wa Kagera. Jina lake halisi ni Anastazia Exavery.

Alianza darasa la kwanza mwaka 2006 ambapo alimaliza darasa la saba mwaka 2013 katika Shule ya Msingi Kalema iliyoko Chato mkoani Geita.

Baada ya kumaliza shule ya msingi hakufanikiwa kuendelea na masomo, hivyo akajikuta akiwa hana hili wala lile pale kijijini kwao. Muigizaji huyu alishawahi kuwa mfanyakazi wa ndani pia kuwa mamantilie.

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ebitoke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.