Donini wa Kaisarea
Mandhari
Donini wa Kaisarea (alifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 307) alikuwa kijana mganga Mkristo ambaye mwanzoni mwa dhuluma ya kaisari Dioklesyano alipelekwa Mismiya kufanya kazi migodini kwa sababu ya imani yake.
Mwaka wa tano, baada ya mateso makali yaliyompata huko, hatimaye kwa amri ya liwali Urbanus, alichomwa moto kwa kuwa alikataa katakata kuikana imani hiyo [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadimishwa tarehe 5 Novemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |