Dimitri Mendeleyev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dmitri Mendeleev)
Rukia: urambazaji, tafuta
Dmitri Mendeleev

Dimitri Ivanovich Mendeleyev (Kirusi Дми́трий Ива́нович Менделе́ев, 8 Februari {kwa K.J. 27 Januari) 1834 mjini Tobolsk2 Februari (K.J. 20 Januari) 1907 mjini Sankt Petersburg) alikuwa mtaalamu wa kemia kutoka nchini Urusi.

Mendeleev alikuwa mtu wa kwanza wa kupanga elementi za kikemia kwa namna ya jedwali la elementi. Baada ya mumaliza jedwali aliweza kutabiri kuwepo kwa elementi tatu zilizogunduliwa baadaye.

Alifuata masomo ya theolojia na ualimu akawa mwalimu wa sayansi shuleni. Aliendelea kusoma kemia huko Paris na Heidelberg akichungulia hasa tabia za gesi.

Baada ya kurudi Urusi alipata nafasi ya kufunsiha kwenye chuo cha teknolojia Sankt Peterburg na pia kwenye chuo kikuu alipoendelea kuwa profesa. Alipatza sifa nyingi kimataifa lakini hakuendelea kupewa nafasi katika akademia ya sayansi kwa sababu ya talaka ya ndoa yake.

1890 alijiuzulu kwenye chuo kikuu kwa sababu alipinga kuingilia kwa serikali katika mambo ya chuo kikuu.

1893 aliombwa kusimamia taasisi ya kusanifisha vipimo ya Urusi. Alianzisha mfumo wa vipimo vya mita nchini akatunga pia kanuni jinsi ya kutengeneza vodka.

Aliaga dunia mwaka 1907. Elementi 101 iliitwa kwa hesima yake "Mendelevi" na pia kasoko ya Mendeleyev kwenye mwezi ilipewa jina kwa kumbukumbu yake.