Dj Davizo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

David William Mchome, maarufu kwa jina la sanaa muziki kama Dj Davizo. alizaliwa 26 Juni 1987, katika wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Ni mwanamuziki wa Bongo Flava kwa miondoko ya dancehall anayefanya shughuli zake za sanaa ya muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, lakini pia ni mtunzi wa mashairi na muandaaji wa ala za muziki kutoka kaskazini mwa Tanzania.[1]

David William Mchome

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa David William Mchome
Pia anajulikana kama Dj Davizo
Amezaliwa 26 Juni 1987
Asili yake Moshi Kilimanjaro, Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava, dancehall
Kazi yake mwanamuziki, mtunzi na Mwandishi
Miaka ya kazi Tangu 2008
Ame/Wameshirikiana na Gigy Money


Elimu na maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

David William Mchome au maarufu kwa jina la Dj Davizo kwenye kazi zake za sanaa ya muziki wa Bongo Flava na Dancehall aliweza kupata elimu yake ya shule ya msingi pamoja na Elimu ya sekondari huko jijini Kampala Uganda na baadaye kurejea nyumbani Moshi Kilimanjaro, Tanzania kwaajili ya maisha mengine pamoja na kuanza safari yake ya sanaa ya muziki nchini Tanzania. Mnamo mwaka 2008 David William Mchome au maarufu kama Dj Davizo aliweza kuunda kundi la kucheza muziki ambalo liliweza kuleta ushindani na mafanikio kipindi cha harakati za kuingia kwenye sanaa ya muziki. Pia David William Mchome au kwa jina la sanaa ya muziki kama Dj Davizo aliweza kupata umaarufu kama Dj mkoani Arusha na jijini Dar es salaam huku akitengeneza ala zake mwenyewe za muziki mpaka kufikia hatua ya kutoa nyimbo iliyoitwa kwa jina la Vumiliaa.[2] iliyoweza kuzidi kumtambulisha kwenye sanaa ya Muziki wa Bongo Flava na miondoko ya dancehall kwa ujumla.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

David William Mchome amekuwa kwenye sanaa ya muziki wa Bongo Flava kwa miondoko ya dancehall pamoja na kazi yake ya awali aliyokuwa akiifanya ya Dj kwa takribani zaidi ya miaka kumi na nne. Huku kwa kipindi hiko chote aliweza kujipatia umaarufu kwa kutoa nyimbo mbalimbali na kupata nafasi ya kushirikiana na wasanii tofauti nchini Tanzania wakiwemo kama Chin Bez, G-nako, Dipper rato, Gigy money. [3]

Vile vile Msanii Dj Davizo amekuwa chini ya uongozi wa Bunduki Music Label ambayo imekuwa ikisimamia kazi zake tangu ajiunge na lebo hiyo ambayo imeleta mafanikio kadhaa kwenye kazi zake za muziki wa Bongo Flava na hususani miondoko anayoifanya ya dancehall hapa nchini Tanzania na pia nje ya mipaka.[4]

Albamu zake[hariri | hariri chanzo]

Mpaka sasa Dj Davizo katika sanaa yake ya muziki wa Bongo Flava kwa miondoko ya dancehall ameweza kutoa albamu zake mbili katika miaka miwili mfululizo ambazo ni kama zifuatazo.

  1. LOD OF MERCY (2021)
  2. POSSITIVEE VIBRATION (2022)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Video Mpya DJ Davizo Ft. Chin Bees, Itazame Hapa (en-US). Global Publishers. Iliwekwa mnamo 2023-05-03.
  2. Video: DJ Davizo, John Rodgers & Shilah – Vumilia – Bongo5.com. bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2023-05-03.
  3. Admin. VIDEO MPYA: G-Nako kashirikishwa kwenye hii “Kinoma noma” ya Dj Davizo (en-US). Millard Ayo. Iliwekwa mnamo 2023-05-03.
  4. Dj Davizo - YouTube. www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2023-05-03.

Viunga vya nje[hariri | hariri chanzo]

Ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Dj Davizo