Devil Kingdom

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Devil Kingdom
Devils KingdomFilamu.jpg
Posta ya Devil Kingdom
Imeongozwa na Steven Kanumba
Imetayarishwa na Steven Kanumba
Imetungwa na Ally Yakuti
Nyota Steven Kanumba
Ramsey Nouah
Kajala Masanja
Fatuma Makongoro
Patcho Mwamba
Imetolewa tar. 26 Aprili, 2011
Ina muda wa dk. 120
Nchi Tanzania
Lugha Kiswahili
Kiingereza

'Devil Kingdom ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2011 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Steven Kanumba, Ramsey Nouah, Kajala Masanja, Fatuma Makongoro na Patcho Mwamba. Filamu imeongozwa na kutayarishwa na Kanumba. Muuswaada andishi umeandikwa na Ally Yakuti. Filamu inahusu kijana mmoja anayehangaika huku na kule bila mafanikio ilahali marafiki zake waliomzunguka wana mafanikio makubwa na wana hela kupita maelezo. Hapa ndipo alipoingizwa katika ulimwengu wa shetani ili awe tajiri kama rafiki zake. [1] Filamu iliingia mtaani rasmi mnamo tarehe 26 Aprili, 2011.[2]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Filamu inaanza na bwana mdogo mmoja mwenye juhudi ya kazi katika maisha lakini hana mafanikio licha ya kujituma vya kutosha. Akiangalia maswahiba zake, mambo swafi na wana mihela hatari. Suala hili linamuumiza kichwa na kupelekea na yeye kutaka kuwa na mafanikio kama wao. Magumu ya maisha yalipelekea kumuuliza Mola wake, ya kwamba huenda asali sana kiasi kwamba inapelekea kutokuwa tajiri kama wale wengine.

Kaanzisha kanisa ili apate chochote kitu, wapi, imedunda hakuna mapato. Siku kaona bora ajitoe ufahamu na kumuuliza mmoja kati ya marafiki zake (Patcho Mwamba) ambao ni mamilionea wamefanyaje hadi wamekuwa hivyo walivyo. Rafiki alifunguka vya kutosha ya kwamba ile si nguvu ya Mungu bali nguvu nyingine za giza ndizo zilizopelekea utajiri wao. Anamweleza ya kwamba ili awe kama wao sharti ajiunge na jumuia ya kisiri kwa mafanikio makubwa.

Anakubaliana na suala hili, wanampa kila kitu, ikiwa ni pamoja na nguvu ya kuponya, hili liliongeza idadi ya wafuasi kanisani mwake, fedha na maisha mazuri lakini inatakiwa arejeshe/atoe sadaka kafara. Ili utajiri wake ubaki kama ulivyo, kuna kipindi anatakiwa atoe kafara ya zeruzeru. Suala hili linamwia vigumu, hivyo basi ile jumuia ya siri inamwambia atoe sadaka wazazi wake badala yake. Baadaye anajaribu kujitoa ili kunusuru wazazi wake, lakini anaambiwa ukiingia katika jumuia hii, hakuna kujitoa tena. Hapa anaamua kwenda kanisani kwake na kumuomba Mungu wake wa kweli.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Devil Kingdom katika Bongo Cinema.com
  2. Devil Kingdom yaingia mtaani rasmi Ijumaa Aprili 26, 2011. Katika Kanumba the Great Blogu.