Lilith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Lilith (Carl Poellath).jpg

Lilith ni jina la mwanamke ambaye katika hadithi fulani za Mesopotamia ya kale anatajwa kama mungu mke.

Biblia inasimulia jinsi dunia ilivyoumbwa na mwanzo wa ubinadamu. Katika maandiko hayo, inasemwa kwamba Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, na baada ya kumuumba Adamu, alichukua ubavu kutoka kwa Adamu na kumuumba Hawa. Ni kweli hadithi za uumbaji zina changamoto kuzifahamu sawasawa, hususani kitabu cha Mwanzo 1:26 na Mwanzo 2. Uumbaji wa mwanamke unatajwa sehemu hizo mbili, lakini kwa namna tofauti, kwa kuwa ni visasili tofauti. Katika Mwa 1:26 Mungu aliwaita wote Adamu na Eva. Katika Mwa 2 Mungu anamuumba Hawa baada ya kuchukua ubavu wa Adamu na kumfanya mwanamke.

Isa 34:14 tu inamtaja Lilith, na jina hilo linatafsiriwa pengine "Bundi", sambamba na wanyama wengine wanaotajwa katika mstari huo na ule unaofuatwa.

Wanaokubali hadithi hiyo wanadai Lilith, si Hawa, ndiye mwanamke wa kwanza ulimwenguni naye aliumbwa na Mungu wakati mmoja na Adamu. Inasemekana kwamba Lilith alifukuzwa na kukataliwa na Mungu baada ya kupatikana kuwa alikuwa mwenye nguvu zaidi na mwenye akili zaidi ya Adamu na hakutii amri za Adamu.

Wanadai Lilith haikutajwa katika kitabu cha Mwanzo kwa kuwa inakwenda kinyume na jadi ya kutaka mnanamke atii mwanamume na wanawake kuwa katika hali ya chini kuliko wanaume. Wanadai pia Biblia ya sasa imepitia vichujio vingi vya kidini ili kuhakikisha kwamba inapoteza baadhi ya sehemu muhimu. Hata hivyo, kuna sehemu ambayo imeachwa ndani yake ambayo inaonyesha kwamba Mungu hakumuumba mwanamume tu bali alimuumba mwanamke kwa wakati huohuo, badala ya simulizi la ubavu kuchukuliwa kutoka kwa Adamu kama ilivyopendekezwa kwenye Biblia.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lilith kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.