Chotara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Familia pana ya kichotara ya Afrika Kusini ikionyesha tofauti katika rangi ya ngozi na nyinginezo.
Barack Obama, rais wa Marekani (2008-2016) ni chotara, kwa sababu baba yake alikuwa Mjaluo wa Kenya na mama alikuwa na asili ya Ulaya.

Chotara (kutoka Kihindi) au shombe ni kiumbe hai ambacho kimetokana na makabila zaidi ya moja ya spishi yake. Kwa mfano, binadamu ambaye alizaliwa na baba Mzungu na mama Mwafrika anaitwa hivyo.[1]

Katika lugha mbalimbali kuna majina maalumu kwa aina za machotara: kwa mfano katika Kihispania kuna Mulato, zambo na mestizo, katika Kireno kuna mulato, caboclo, cafuzo, ainoko na mestiço.

Pengine sensa zinauliza asili ya wakazi, zikiacha nafasi ya kutaja asili zaidi ya moja.

Tanbihi

  1. "Not surprisingly, chemomedical scientists are divided in their opinions about race. Some characterize it as 'biologically meaningless' or 'not based on scientific evidence', whereas others advocate the use of race in making decisions about medical treatment or the design of research studies." Lynn B. Jorde; Stephen P. Wooding (2004). "Genetic variation, classification and 'race'". Nature Genetics 36 (11 Suppl): S28–S33. PMID 15508000. doi:10.1038/ng1435.  citing Guido Barbujani; Arianna Magagni; Eric Minch; L. Luca Cavalli=Sforza (April 1997). An apportionment of human DNA diversity. Proceedings of the National Academy of Sciences USA 94. ku. 4516–4519.  Check date values in: |date= (help).

Marejeo

Viungo vya nje

  • The Multiracial Activist, an online activist publication registered with the Library of Congress, focused on multiracial individuals and interracial families since 1997
  • ProjectRACE, an organization leading the movement for a multiracial classification
Asasi za kutetea haki za binadamu