Chanjo ya Homa ya Manjano A
Vaccine description | |
---|---|
Target disease | Hepatitis A |
Aina | ? |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Biovac A, Havrix, Vaqta, others |
AHFS/Drugs.com | Kigezo:Drugs.com |
MedlinePlus | a695003 |
Kategoria ya ujauzito | B2(AU) C(US) Safety undetermined, risk likely low |
Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Intramuscular |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | J07BC02 |
ChemSpider | noneKigezo:Chemspidercite |
(hii ni nini?) (thibitisha) |
Chanjo ya Homa ya Manjano A ni chanjo ambayo huzuia Homa ya Manjano A.[1] Ni faafu kwa karibu 95% ya hali na hudumu kwa angalau miaka kumi na mitano na ikiwezekana kwa maisha yote ya mtu.[1][2] Ikitolewa, vipimo viwili vinapendekezwa kuanzia baada ya umri wa mwaka mmoja. Hutolewa kwa kudunga sindano kwenye misuli.[1]
Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza chanjo ya ulimwenguni katika maeneo ambayo ugonjwa huo ni wa kawaida. Mahali ambapo ugonjwa huu ni kawaida sana, chanjo ya kuenea kila pahali haipendekezwi kwani watu wote hupata kingamwili kupitia kwa uambukizi wakiwa watoto.[1] Kituo cha Udhibiti na Kinga dhidi ya Magonjwa (CDC) kinapendekeza kuwapa chanjo watu wazima walio kwenye hatari sana na watoto wote.[3]
Athari kuu ni nadra sana. Uchungu katika sehemu iliyodungwa sindano hutokea kwa karibu 15% ya watoto na nusu ya watu wazima. Chanjo nyingi za Homa ya Manjano A huwa na virusi visivyo tendaji huku chache huwa na virusi hafifu. Zile zenye virusi hafifu hazipendekezwi wakati wa ujauzito au kwa wale walio na kinga duni mwilini. Uundaji chache huunganisha homa ya manjano A na ama chanjo ya homa ya manjano B au ya homa ya matumbo.[1]
Chanjo ya kwanza ya Homa ya manjano A iliidhinishwa Ulaya mwaka wa 1991 na Marekani mwaka wa 1995.[4] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Duniani, dawa muhimu zaidi inayohitajika kwenye mfumo wa kimsingi wa afya.[5] Gharama yake Marekani ni kati ya dola 50 na dola 100.[6]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "WHO position paper on hepatitis A vaccines – June 2012" (PDF). Wkly Epidemiol Rec. 87 (28/29): 261-76. 2012 Jul 13. PMID 22905367.
- ↑ Ott JJ, Irving G, Wiersma ST (December 2012). "Long-term protective effects of hepatitis A vaccines. A systematic review". Vaccine. 31 (1): 3–11. doi:10.1016/j.vaccine.2012.04.104. PMID 22609026.
- ↑ "Hepatitis A In-Short". CDC. July 25, 2014. Retrieved 7 December 2015.
- ↑ Patravale, Vandana; Dandekar, Prajakta; Jain, Ratnesh (2012). Nanoparticulate drug delivery perspectives on the transition from laboratory to market (1. publ. ed.). Oxford: Woodhead Pub. p. 212. ISBN 9781908818195.
- ↑ "19th WHO Model List of Essential Medicines (April 2015)" (PDF). WHO. April 2015. Retrieved May 10, 2015.
- ↑ Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. p. 314. ISBN 9781284057560.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano A kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |