Céline Dion

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Celine Dion)
Jump to navigation Jump to search
Céline Dion
Dion akiimba wimbo wa "Taking Chances" wakati wa "Ziara ya Céline Dion ya Taking Chances" Concert lililofanyika Bell Centre, Montreal, Kanada mnam tar. 19 Agosti 2008.
Dion akiimba wimbo wa "Taking Chances" wakati wa "Ziara ya Céline Dion ya Taking Chances" Concert lililofanyika Bell Centre, Montreal, Kanada mnam tar. 19 Agosti 2008.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Céline Marie Claudette Dion
Amezaliwa 30 Machi 1968 (1968-03-30) (umri 50)
Charlemagne, Quebec, Kanada
Asili yake Montreal, Quebec, Kanada
Aina ya muziki Pop, rock
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo[1]
Ala sauti
Aina ya sauti Soprano[2]
Miaka ya kazi 1980–2000, 2002-hadi leo
Studio 550/Epic/Sony (1986–2004)
Epic (2004–2007)
Sony Music Entertainment/Columbia (2007-hadi leo)
Tovuti www.celinedion.com

Céline Dion (amezaliwa tar. 30 Machi 1968) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo mashuhuri za pop kutoka nchini Kanada. Alizaliwa katika mji wa Charlemagne mjini Quebec, Kanada. Yeye ni mdogo kuzaliwa katika familia ya watoto kumi na nne.

Alifikisha umri wa miaka 12, kaka yake alimpeleka kwa meneja wa urekodi aliyejulikana kwa jina la René Angélil, ambaye baadaye akaja kumwoa na kumzalia mtoto.

Dion alipokuwa na miaka 18

Kwa msaada wake, alifanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza mnamo mwaka wa 1981, ambazo alikuwa akiimba kwa Kifaransa. Alitoa albamu yake ya kwanza kwa lugha ya Kiingereza kunako mwaka wa 1990.

Kwa sasa anaishi mjini Las Vegas ambapo alifanya maonyesho yake mengi sana. Mnamo mwaka wa 2007, aliimba katika onyesho moja akiwa na Elvis Presley, ambalo liliandaliwa katika kompyuta ambazo kuna picha za maonyesho ya zamani yaliyofanywa na Elvis. Dhumuni la onyesho, lilikuwa likiandaliwa kwa ajili ya onyesho la TV la American Idol.

Ameuza albamu babkubwa duniani kwa msanii wa kike, kitendo ambacho kimemfanya ashinde Tuzo za Muziki wa Dunia kunako mwaka wa 2004. Pia ameuza zaidi ya nakala milioni 7 za muziki kwa lugha ya Kifaransa.

Amekuwa nyota maarufu kwa Ulaya kwa albamu yake ya Incognito ya mwaka wa 1987. Baada ya hapo, akafanya maonyesho kadhaa katika Ulaya kisha akaja kuwa maarufu zaidi.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Albamu zake kwa lugha ya Kiingereza[hariri | hariri chanzo]

Albamu zake kwa lugha ya Kifaransa[hariri | hariri chanzo]

 • 1981: La Voix du bon Dieu
 • 1981: Céline Dion chante Noël
 • 1982: Tellement j'ai d'amour...
 • 1983: Les Chemins de ma maison
 • 1983: Chants et contes de Noël
 • 1984: Mélanie
 • 1985: C'est pour toi
 • 1987: Incognito
 • 1991: Dion chante Plamondon
 • 1995: D'eux
 • 1998: S'il suffisait d'aimer
 • 2003: 1 fille & 4 types
 • 2007: D'elles

Single zake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Single Nafasi iliyoshika
CAN U.S. UK FRA
1990 "Where Does My Heart Beat Now" 6 4 72 20
1992 "If You Asked Me To" 3 4 57
"Beauty and the Beast" (akiimba na Peabo Bryson) 2 9 9
1993 "The Power of Love" 1 1 4 3
"Un garçon pas comme les autres (Ziggy)" 2
1994 "Think Twice" 14 95 1
1995 "Pour que tu m'aimes encore" 7 1
"Je sais pas" 1
"Because You Loved Me" 1 1 5 19
1996 "It's All Coming Back to Me Now" 2 2 3 13
"All by Myself" 4 6 5
1997 "[:en:[Tell Him (Barbra Streisand and Celine Dion song)|Tell Him]]" (akiimba na Barbra Streisand) 12 3 4
1998 "The Reason" 11 1
"My Heart Will Go On" 14 1 1 1
"Immortality"(akiimba na Bee Gees) 5 15
"I'm Your Angel" (akiimba na R. Kelly) 37 1 3 97
"S'il suffisait d'aimer" 4
2000 "I Want You to Need Me" 1
2001 "Sous le vent" (akiimba Garou) 14 1
2002 "A New Day Has Come" 2 22 7 23
2003 "I Drove All Night" 1 45 27 22
"Tout l'or des hommes" 2 3
2005 "Je ne vous oublie pas" 2
2007 "Et s'il n'en restait qu'une (je serais celle-là)" 1

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Britannica.com. Céline Dion. Retrieved 13 Januari 2006.
 2. Review/Pop; The International Sound of Céline Dion. The New York Times. 2 Machi 1994. Retrieved 17 Novemba 2008

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Céline Dion kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.