Carlos Fernández

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Carlos Fernandez.

Carlos Fernández Luna (alizaliwa Seville, Andalusia, Mei 22, 1996) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Sevilla FC.

Fernández alianza kucheza soka na timu Sevilla FC akiwa na umri wa miaka 17, akishindana katika Segunda División B. Tarehe 18 Desemba 2013, alihamishwa kutoka Sevilla B na kupelekwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Fernández alifunga goli lake la kwanza na Sevilla A mnamo 21 Agosti 2016, katika uwanja wa nyumbani kwa kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Girona FC. Wakati wa mafunzo mwanzoni mwa Oktoba 2016, Fernández alivunjika sehemu ya goti la mguu wa kushoto, akipoteza msimu wote.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carlos Fernández kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.