Nenda kwa yaliyomo

Bweni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa matumizi tofauti ya neno hili tazama Bweni (Pangani)

Bweni la wavulana katika shule ya Australia mnamo 1898
Chumba cha bweni kwa wanafunzi wawili, mnamo 2008, chuo jimboni Maryland, Marekani

Bweni (kwa Kiingereza dormitory) ni nyumba ya kulala hasa kwa ajili ya wanafunzi wa chuo au shule.

Kuna mabweni sahili ambako vitanda vya ghorofa vinapatikana kwa kundi la wanafunzi wanaolala pamoja katika chumba kimoja. Mabweni yanahitaji kuwa na vyoo, bafu na kabati za kuwekea nguo na vitu vya binafsi kila mwanafunzi. Majengo ya mabweni huwa pia na jiko na ukumbi wa chakula.

Mabweni mazuri zaidi huwa na vyumba vidogo ambako si zaidi ya wanafunzi 2-3 wanaoshirikiana nafasi ya chumba kimoja, wakati mwingine pia na chumba kidogo cha bafu na choo.

Katika shule na vyuo mbalimbali wanafunzi wote hutakiwa kukaa bwenini, katika shule nyingine wanafunzi wanaweza kuchagua na tena kuna shule pasipo na bweni.

Mara nyingi wanafunzi wanaingia katika mabweni ya pekee kufuatana na jinsia yaani wanafunzi wa kike na wa kiume. Kuna pia mabweni kwenye vyuo vikuu ambako hawatenganishwi, hasa kama kila mwanafunzi anapata chumba chake cha pekee.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: