Bwana wa Mapete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bwana wa Mapete ni kichwa cha kitabu cha bunilizi ya kinjozi kilichoandikwa na J.R.R. Tolkien.

Kwa asili, Tolkien alikiandika kama mfuatano wa kitabu chake cha Mhobiti kilichokuwa kimetolewa mwaka 1937. Ila Bwana wa Mapete ikaendelea kuwa riwaya kubwa katika juzuu tatu. Tolkien aliiandika kati ya miaka 1937 na 1949, hasa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Hatimaye juzuu hizo tatu zilitolewa kama vitabu vitatu kuanzia 1954 hadi 1955.

Tangu kutolewa, Bwana wa Mapete imetafsiriwa katika lugha nyingi na imekuwa kitabu muhimu katika fasihi ya karne ya 20.

Kichwa cha kitabu hicho chamrejea mpinzani wa hadithi aitwaye Sauron; yeye alikuwa ameumba Pete Kuu ili kutawala Dunia ya Kati nzima. Hadithi ya kitabu yasimulia jinsi mashujaa wanavyompigania Sauron vita. Baadhi ya mashujaa hasa ni wahobiti wanne: Frodo Baggins, Samwise Gamgee (Sam), Meriadoc Brandybuck (Merry) na Peregrin Took (Pippin).

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bwana wa Mapete kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.