Bustani ya wanyama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Matiger kwenye bustani ya wanyama
Kitengo cha Panda kwenye bustani ya wanyama ya Chiang Mai (Uthai)
Wageni wanalisha na kushika panyabuku waliozoea binadamu kwenye bustani ya wanyama ya Parc Animalier des Pyrenées, Ufaransa
Twiga za Kiafrika huko Melbourne, Australia

Bustani ya wanyama ni mahali ambapo wanyama hasa wanyamapori wa aina mbalimbali wanatunzwa ili watu wapate kuwatazama.

Siku hizi bustani ya wanyama zimekuwa pia mahali pa kutunza spishi au aina za wanyama walioko hatarini kutokomea.

Miji mingi mikubwa duniani ina bustani zaa wanyama. Katika baadi ya bustani hizi watu hulipa kiingilio wakitaka kuingia. Lakini hata hivyo bustani hizi hazipokei mapato ya kutosha hivyo hazina budi kupokea pia misaada kutoka serikali.

Umuhimu wa bustani za wanyama ni katika

  • kuwapatia watu nafasi ya kuona kwa macho yao wanyama wa nchi zilizo mbali
  • kuwaelimisha watu juu ya wanyama wa dunia pia kuhusu mazingira yao
  • kuwa kituo cha utafiti wa kisayansi kuhusu wanyama
  • kuhifadhi na kufuga aina za wanyama hatarini kutokomea hasa wasio na mazingira asilia tena

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: