Bukayo Saka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bukayo Saka

Bukayo Ayoyinka T. M. Saka (alizaliwa Ealing, Greater London, 5 Septemba 2001)[1] ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anacheza kama winga kwa klabu ya Arsenal FC.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Saka ana asili ya Nigeria kwani wazazi wake wote ni wenyeji wa Nigeria waliohamia Uingereza kikazi. Jina lake Bukayo ni la kiasili linalomaanisha "Ongezeko la furaha" katika lugha ya kabila la Wayoruba linalopatikana kusini mwa Nigeria.

Saka alisoma shule ya msingi ya Edward Betham CofE ambapo baadae alijiunga na sekondari ya Greenford.

Saka alisikika akisema baba yake mzazi ndiye chachu au hamasa kubwa ya mafanikio yake kwani amekuwa bega kwa bega tangu mwanzo wa maisha yake ya mpira wa miguu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bukayo Saka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.