Nenda kwa yaliyomo

Blackheads

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Blackheads katika uso.

Blackheads (kutoka Kiingereza; pia "comedo" kwa lugha hiyo) ni aina ya chunusi ambayo huonekana kwa mtu wakati ngozi yake yapata maaafa na haitibiwi kwa wakati unaofaa. Unapopata jeraha la ngozi, mwili wako hujaribu kila uwezalo ili kutibu jeraha lile. Unaposhindwa kufanya hivi kwa wakati unaofaa, tishu ya ngozi hutengenezwa mahala pale ambayo huwa na ile rangi nyeusi na ndiyo maana mtu huonekana kana kwamba ana ngozi nyeusi.

Blackheads huathiri wapi[hariri | hariri chanzo]

Blackheads huathiri mahali popote mwilini, bora tu pawe na ngozi inayoweza kupata jeraha. Blackheads sanasana huonekana kwa uso ambapo anaye blackheads hujipata na kiwango kidogo sana cha kujithamini maaana ngozi yake imepata chunusi. Huenda mtu akawa pia anahisi uchungu pahala ambapo kuna blackheads. Blackheads pia zaweza kupatikana katika mgongo.

Matibabu ya blackheads[hariri | hariri chanzo]

Unapopata blackheads katika mgongo, daktari atakushauri utumie dawa za Benzoyl peroxide ambazo huwa na nguvu nyingi sana za kuondoa zile blackheads. Hata hivyo, hutaweza kutumia dawa hii kutibu blackheads kwa uso maana ngozi ya uso ni nyororo na huenda ikaathirika pakubwa na nguvu za dawa hii. Daktari wako atakupa dawa inayofaa kwa blackheads za uso.

Kujikinga kutokana na blackheads[hariri | hariri chanzo]

Wanawake ndio sanasana hupatwa na blackheads kwa sababu ya kutumia vipodozi kadha wa kadha. Ili kujikinga kutokana na majeraha ya ngozi inayoleta blackheads, ni vizuri uhakikishe kwamba watumia vipodozi visivyo na kemikali nyingi sana, usafishe ngozi yako kwa maji safi na sabuni ya kuaminika, nyoa nywele zilizo usoni kwa uangalifu pamoja na kula lishe bora ambayo haitaathiri ngozi yako. Makala mengine yaonyesha kwamba kuna udongo wa Kihindi unaoweza ukaponya chunusi hizi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Blackheads kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.