Nenda kwa yaliyomo

Bipolar Disorder

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emil Kraepelin.mtafiti wa Bipola Disoder

Tatizo la kubadilika kwa hisia, kama kufurahi na kuhuzunika kupita kiasi, ni tatizo la kiakili ambalo husababisha misimu ya huzuni na misimu ya furaha zisizo za kawaida.[1][2][3]

Ufafanuzi

[hariri | hariri chanzo]

Hisia zilizozidi ni muhimu na zinajulikana kama wazimu mkali, kwa kutegemea ukali wake, au iwapo dalili za wendawazimu zinaonekana.[1] Wakati wa wazimu, tabia ya mtu hufanya au huhisi kwa namna yenye nguvu, furaha au hasira isiyo ya kawaida.[1] watu binafsi mara nyingi hufanya maamuzi bila kufikiria vizuri na bila kujali sana matokeo[2] Haja ya kulala huwa imepungua wakati wa hatua za wazimu.[2] Wakati wa vipindi vya huzuni, kunaweza kuwa na kulia, mtazamo hasi kuhusu maisha, na kutoangalia wengine kwa macho.[1] Hatari ya kujiua miongoni mwa walio na ugonjwa huo ipo juu zaidi ya asilimia 6 kwa zaidi ya miaka 20, huku kujiumiza hutokea kwa asilimia 30 na 40.[1] Masuala mengine ya afya ya kiakili kama vile tatizo la kuwa na wasiwasi na tatizo la kiakili la matumizi mabaya ya vifaa au dawa ili kuathiri hisia za mtu mara nyingi huhusishwa na tatizo la kubadilika kwa hisia.[1]

Sababu na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo havifahamiki vyema, lakini vipengele vya mazingira na jenetikia huchangia.[1] Jeni nyingi za athari kidogo huchangia hatari.[1][4]

Vipengele vya hatari ya kimazingira vinajumuisha historia ya unyanyasaji utotoni na mawazo ya muda mrefu.[1] Karibu 85% ya hatari ni ya kurithi.[5] Hali hiyo inaainishwa kama tatizo linalosababisha kubadilika kwa hisia I iwapo kumekuwa na angalau kisa kimoja cha wazimu, na au bila visa vya huzuni, na kama tatizo linalosababisha kubadilika kwa hisia II iwapo kumekuwa na angalau kisa kimoja cha wazimu kali (lakini bila visa vya wazimu) na kisa kimoja kikuu cha huzuni.[2] Kwa wale walio na dalili zisizo kali sana kwa muda mrefu, hali hiyo tatizo la huzuni na furaha kupita kiasi linaweza kupatikana.[2] Iwapo dalili ni kwa sababu ya dawa au shida za matibabu, inaoanishwa tofauti.[2]

Hali nyingine ambazo zinaweza kujitokeza sawa ni pamoja na tatizo la upungufu na uharibifu wa umakini, tatizo la kiakili lenye kuleta wazo na tendo lisilobanduka, matatizo ya kiakili yenye kuleta mtazamo, fikra, tabia na mhemko usio wa kawaida (skizofrenia) na tatizo la kiakili lenye kuleta matumizi mabaya ya vifaa au dawa ili kuathiri hisia za mtu, sawa na idadi kubwa ya hali ya matibabu.[1]

Kupimwa kwa ajili ya matibabu hakuhitajiki kwa utambuzi, ingawa vipimo vya damu au picha za matibabu zinaweza kufanywa ili kuondoa matatizo mengine.[6]

Tiba na matarajio yake

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu kwa kawaida hujumuisha matibabu ya kisaikolojia sawa na dawa kama vile vidhibiti hisia na dawa ya kuzuia magonjwa ya kiakili.[1] Mifano ya vidhibiti hisia ambazo hutumika kwa kawaida inajumuisha lithiamu na dawa ya kuzuia ugonjwa wa misukosuko mbalimbali.[1] Kutibiwa bila kujua katika hospitali ya magonjwa ya akili kunaweza kutakikana ikiwa mtu ni hatari kwake mwenyewe au kwa watu wengine japo anakataa matibabu.[1] Shida hatari za kitabia, kama vile uchochezi na ugomvi, zinaweza kudhibitiwa kwa dawa za kuzuia magonjwa ya akili kwa muda mfupi au dawa ya kutibu wasiwasi (benzodiazepini).[1] Wakati wa vipindi vya wazimu, inapendekezwa kuwa dawa za kumaliza huzuni zisitishwe.[1] Ikiwa dawa za kumaliza huzuni zitatumika kwa vipindi vya huzuni, zinafaa kutumika pamoja na dawa za kudhibiti hisia.[1]

Tiba ya msukomsuko kielektroniki (ECT), japo haijasomwa sana, inaweza kujaribiwa kwa wale ambao hawaathiriki na matibabu mengine.[1] Ikiwa matibabu yatasitishwa, inapendekezwa kuwa hii ifanywe polepole.[1] Watu wengi wana shida za kifedha, kijamii au za kikazi kwa sababu ya ugonjwa huu.[1] Matatizo haya hutokea kwa robo au thuluthi moja ya wakati, kwa wastani.[1] Kwa sababu ya chaguo baya la maisha na athari mbaya za dawa, hatari ya kifo kutoka kwa vyanzo vya asili kama vile ugonjwa wa moyo ni mara mbili ya hatari ya idadi ya kawaida ya watu.[1]

Tatizo linalosababisha kubadilika kwa hisia huathiri takriban 1% ya idadi ya watu ulimwenguni.[7] Katika Marekani, karibu 3% wanakadiriwa kuathiriwa kwa wakati fulani maishani mwao; viwango vinaonekana kuwa sawa kwa jinsia ya kike na ya kiume.[8]

Umri wa kawaida zaidi ambao dalili huanza ni umri wa miaka 25.[1] Gharama ya kiuchumi ya tatizo hili inakadiriwa kuwa dola bilioni 45 kwa Marekani mwaka wa 1991.[9] Sehemu kubwa ya hii ilihusiana na idadi ya juu ya siku ambazo watu walikosa kwenda kazini, zinakadiriwa kuwa 50 kwa mwaka.[9] Watu walio na tatizo linalosababisha kubadilika kwa hisia mara nyingi hukumbana na shida za unyanyapaa wa kijamii.[1]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 1.21 1.22 Anderson IM, Haddad PM, Scott J (Des 27, 2012). "Bipolar disorder". BMJ (Clinical research ed.). 345: e8508. doi:10.1136/bmj.e8508. PMID 23271744.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 American Psychiatry Association (2013). Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders (toleo la 5th). Arlington: American Psychiatric Publishing. ku. 123–154. ISBN 0-89042-555-8.
  3. "DSM IV Criteria for Manic Episode". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 31, 2017. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Goodwin, Guy M. "Bipolar disorder". Medicine. 40 (11): 596–598. doi:10.1016/j.mpmed.2012.08.011.
  5. Charney, Alexander; Sklar, Pamela (2018). "Genetics of Schizophrenia and Bipolar Disorder". Katika Charney, Dennis; Nestler, Eric; Sklar, Pamela; Buxbaum, Joseph (whr.). Charney & Nestler's Neurobiology of Mental Illness (toleo la 5th). New York: Oxford University Press. uk. 162.
  6. NIMH (Aprili 2016). "Bipolar Disorder". National Institutes of Health. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 27, 2016. Iliwekwa mnamo Agosti 13, 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  7. Grande, I; Berk, M; Birmaher, B; Vieta, E (Aprili 2016). "Bipolar disorder". Lancet (Review). 387 (10027): 1561–72. doi:10.1016/S0140-6736(15)00241-X. PMID 26388529.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Diflorio, A; Jones, I (2010). "Is sex important? Gender differences in bipolar disorder". International Review of Psychiatry (Abingdon, England). 22 (5): 437–52. doi:10.3109/09540261.2010.514601. PMID 21047158.
  9. 9.0 9.1 Hirschfeld, RM; Vornik, LA (Juni 2005). "Bipolar disorder–costs and comorbidity". The American journal of managed care. 11 (3 Suppl): S85–90. PMID 16097719.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Jua habari zaidi kuhusu Bipolar Disorder kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi
Vitabu kutoka Wikitabu
Dondoo kutoka Wikidondoa
Matini za vyanzo kutoka Wikichanzo
Picha na media kutoka Commons
Habari kutoka Wikihabari
Vyanzo vya elimu kutoka Wikichuo