Berkari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Berkari (pia: Berchaire, Bererus; Akwitania, leo nchini Ufaransa, 620 - Montier-en-Der, leo nchini Ufaransa, 685/696) alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki, aliyeunganisha desturi za Kolumbani na za Benedikto kwa monasteri ambazo alizianzisha na kuziongoza.

Siku ya Alhamisi kuu aliuawa kwa kisu na mtawa mbaya aliyekuwa amefukuzwa naye. Mwenyewe alimsamehe akafariki Jumapili ya Pasaka.[1]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Machi[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Patrick Corbet, Les moines du Der 673-1790, Dominique Guéniot, 2003
  • Charles Lalore, Polyptyque de Montier-en-Der, éd Charles Lalore, Paris, 1878
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.