Mchekwa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Bauhinia)
Mchekwa (Bauhinia spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mchekwa mwekundu
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi zaidi ya 500, 7 katika Afrika ya Mashariki: |
Michekwa (Bauhinia spp.) ni vichaka au miti ya familia Fabaceae na kuna zaidi ya spishi 500. Jina hili hutumika kwa Piliostigma thonningii pia lakini spishi hii ina majina mengi mengine (angalia mchekeche).
Michekwa inatokea misituni kwa kanda za tropiki za Afrika, Amerika na Asia lakini spishi kadhaa zinatokea katika savana au nusujangwa. Majani yao yana umbo la unyayo wa ngamia. Maua yao ya sm 7.5-12.5 yana petali tano zenye rangi ya nyeupe, njano, nyekundu, pinki au zambarau.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Bauhinia acuminata, Mchekwa Mweupe
- Bauhinia kalantha, Mchekwa wa Kalahari
- Bauhinia petersiana, Mchekwa wa Peters au Mgobwali
- Bauhinia purpurea, Mchekwa Zambarau
- Bauhinia racemosa, Mchekwa Maua-vishada
- Bauhinia tomentosa, Mchekwa Njano, Msabuni au Msaponi
- Bauhinia variegata, Mchekwa Mwekundu
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Maua na majani ya mchekwa mweupe
-
Ua la mchekwa zambarau
-
Maua ya mchekwa maua-vishada
-
Ua la mchekwa njano
-
Ua la mchekwa mwekundu
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mchekwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |