Bata bukini mabawa-kijani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bata bukini mabawa-kijani
Bata bukini mabawa-kijani akijilisha
Bata bukini mabawa-kijani akijilisha
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na nasaba na bata)
Nusufamilia: Plectropterinae
Jenasi: Plectropterus
Stephens, 1824
Spishi: Plectropterus gambensis
(Linnaeus, 1766)
Ngazi za chini

Nususpishi 2:

Bata bukini mabawa-kijani (Plectropterus gambensis) ni ndege wa maji na spishi pekee katika nusufamilia Plectropterinae ya familia Anatidae. Anatokea Afrika kusini kwa Sahara tu.

Ndege huyo ni ndege wa maji mkubwa kabisa duniani. Urefu wake ni sm 75-115 na uzito ni kg 4-6.8 (kwa nadra hadi kg 10). Madume ni wakubwa kuliko majike na nususpishi P. g. niger ni mdodo kuliko P. g. gambensis. Upana wa mabawa ni sm 150-200. Rangi yao inaonekana nyeusi kutoka mbali, lakini kutoka karibu mng'ao kijani unaweza kuonwa. Ndege akiruka mabaka makubwa meupe yanaonekana kwenye mbele ya mabawa. Domo na miguu ni myekundu na madume wana paji jekundu pia.

Nususpishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu ndege fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bata bukini mabawa-kijani kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.