Bata bukini mabawa-kijani
Mandhari
(Elekezwa kutoka Plectropterus gambensis)
Bata bukini mabawa-kijani | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bata bukini mabawa-kijani akijilisha
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nususpishi 2:
|
Bata bukini mabawa-kijani (Plectropterus gambensis) ni ndege wa maji na spishi pekee katika nusufamilia Plectropterinae ya familia Anatidae. Anatokea Afrika kusini kwa Sahara tu.
Ndege huyo ni ndege wa maji mkubwa kabisa duniani. Urefu wake ni sm 75-115 na uzito ni kg 4-6.8 (kwa nadra hadi kg 10). Madume ni wakubwa kuliko majike na nususpishi P. g. niger ni mdodo kuliko P. g. gambensis. Upana wa mabawa ni sm 150-200. Rangi yao inaonekana nyeusi kutoka mbali, lakini kutoka karibu mng'ao kijani unaweza kuonwa. Ndege akiruka mabaka makubwa meupe yanaonekana kwenye mbele ya mabawa. Domo na miguu ni myekundu na madume wana paji jekundu pia.
Nususpishi
[hariri | hariri chanzo]- Plectropterus gambensis
Picha
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu ndege fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bata bukini mabawa-kijani kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |