Basilika kuu la Bikira Maria
Mandhari
Basilika kuu la Bikira Maria (kwa Kiitalia: Santa Maria Maggiore) katika mtaa wa Esquilino jijini Roma ni kanisa lililojengwa kwanza na Papa Liberius (352-366) kwa heshima ya Bikira Maria .
Kama lilivyo sasa ni kazi hasa ya Papa Sixtus III (432–440) aliyelishughulikia mara baada ya huyo kutangazwa na Mtaguso wa Efeso (431) kuwa Mama wa Mungu[1].
Hii inabaki kweli ingawa sehemu nyingine zilijengwa upya, hasa baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 1348.
Kanisa hilo lina cheo cha Basilika, tena Basilika la Kipapa.
Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Agosti[2].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Basilika kuu la Bikira Maria kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |