Baaba Maal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Baaba Maal
Taarifa za usuli
Amezaliwa12 Novemba 1953 (1953-11-12) (umri 70)
Podor, French West Africa
(now Senegal)
Aina
Kazi yake
Ala
Miaka ya kazi1989–mpaka sasa
Lebo
Wavutibaabamaal.com

Baaba Maal (amezaliwa 12 Novemba 1953) ni mwaimbaji na mpigaji gitaa kutoka nchini Senegal. Baaba Maal alizaliwa mjini Podor, karibu na Mto Senegal. Anafahamika sana ndani na nje ya Afrika akiwa kama mwanamuziki maarufu mno kutoka nchini humo, Senegal. Mbali na kuweza kupiga gitaa kavu, pia anaweza kupiga tumba. Mpaka sasa, ametoa albamu kadhaa , akiwa na lebo na nyingine za kujitegemea. Mwezi wa Julai 2003, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa upande wa vijana.[1]

Maal huimba kwa Kipular[2] na huhesabiwa kama mchocheaji wa kimila wa Wapula, ambao walikuwa wakiishi pembezoni mwa Mto Senegal katika dola la kale la Kisenegali la Futa Tooro.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Maal alitarajiwa kufuata nyayo za babaye za kuwa mvuvi. Hata hivyo, athira ya rafiki yake wa kitambo na mwimbaji, mhadithiaji wa familia, mpigaji gitaa kipofu Mansour Seck, Maal akajidhatiti katika kujifunza muziki kutoka kwa mamaye na mwalimu wake mkuu wa shule alokuwa anasoma wakati huo. Baadaye alienda kujiendeleza kimasomo zaidi katika chuo kikuu cha Dakar kabla ya kupata ufadhili wa masomo katika chuo cha sanaa cha mjini Paris, Ufaransa, Beaux-Arts in Paris.[onesha uthibitisho]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kurudi masomoni mjini Paris, Maal alijifunza muziki wa asili kutoka kwa Mansour Seck na kuanza kutumbuiza na bendi ya Daande Lenol. Mchanganyiko wa kimuziki wa Maal ulisonga mbele zaidi baada ya miaka kumi kwa kuchanganya kwake muziki wa reggae, chalanga na Breton katika albamu yake ya mwaka wa 1994, Firin' in Fouta. Katika mchanganyiko huo aliweza kuumba mtindo wa kipekee uliopelekea kuanzishwa kwa kundi la waghani Positive Black Soul na Afro Celt Sound System. Mchanganyo wake uliendelea hadi katika albamu yake ya mwaka 1998 Nomad Soul, ambayo alikuwamo Brian Eno akiwa kama mmoja kati ya watayarishaji saba wa albamu hiyo. Miongoni mwa matoleo yake ya kujitegemea, alichangia nyimbo mbili, "Bushes" na "Dunya Salam", katika wazo la albamu ya 1 Giant Leap.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Maal akitumbuiza atika tamasha la Opening Plenary huko mjini New Theatre, mnamo Machi 2011

Albumu[hariri | hariri chanzo]

 • 1989 – Passion – Sources (kompilesheni) - Real World Records
 • 1989 – Djam Leelii (akiwa na Mansour Seck) – Mango Records
 • 1991 – Baayo (akiwa na Mansour Seck) – Mango
 • 1992 – Lam Toro – Mango
 • 1994 – Wango – Syllart
 • 1994 – Firin' in Fouta – Mango
 • 1995 – Gorel – 4th & Broadway
 • 1997 – Taara – Melodie
 • 1998 – Nomad Soul – Import
 • 1998 – Djam Leelii: The Adventurers – Yoff Productions
 • 2000 – Jombaajo – Sonodisc
 • 2001 – Missing You (Mi Yeewnii) – Palm
 • 2003 – The Best of the Early Years (compilation) – Wrasse
 • 2005 – Palm World Voices: Baaba Maal (compilation) – Palm
 • 2008 – On The Road (kompilesheni) – Palm
 • 2009 – Television – Palm
 • 2016 – The Traveller – Palm / Marathon Artists

Matoleo ya Import[hariri | hariri chanzo]

 • Jombaajo
 • Ngalanka
 • Ndilane

Msanii mchangizi[hariri | hariri chanzo]

DVD[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Chinen, Nate. "Exhilarating and Aware, an Eclectic Advocate", The New York Times, 4 July 2006. (en) 
 2. Romer, Megan. "Baaba Maal Profile and Biography - Learn More About Senegalese African Musician Baaba Maal". Worldmusic.about.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-06. Iliwekwa mnamo 2016-01-15.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
 3. "Baaba Maal Tunes In With Brazilian Girls On 'Television'". Billboard. 
 4. "'Johannesburg' with Baaba Maal, The Very Best & Beatenberg". 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]