Aurlus Mabele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aurlus Mabélé (24 Oktoba 195319 Machi 2020) alikuwa mtunzi na mwimbaji kutoka Jamhuri ya Kongo.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mabele alizaliwa katika mji wa Brazzaville, wilayani Poto-Poto nchini Jamhuri ya Kongo. Jina lake halisi lilikuwa Aurélien Miatsonama. Alianzisha kundi liitwalo "Ndimbola Lokole".

Baada ya kushiriki sana barani Ulaya, mwaka 1986 yeye na Diblo Dibala na Mav Cacharel, wakaanzisha kundi la Loketo. Kwa pamoja wakatengeneza muziki maarufu wa soukous ambapo baadaye akatajwa kama mfalme, hivyo basi ikapelekea msemo wa kuwa "Aurlus Mabele ndiye mfalme wa soukous".

Katika miaka 25 ya kazi zake ameuza zaidi ya nakala milioni 10 za albamu dunia nzima na alisaidia kwa kiasi kikubwa katika kuitambulisha na kuisukuma vilivyo muziki wa soukous nje ya mipaka ya bara la Afrika. Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza kwa miaka mitano, lakini aliweza kujipanga ili kufanya matamasha na kundi zima la Loketo huko Ulaya kati ya mwezi Mei na Juni, 2009.

Kwa kushirikiana na wapiga gitaa maarufu na wenye vipaji, ametengeneza dansi ya Kiafrika yenye ladha yake ya kipekee ya soukous kwa kutunga nyimbo kama vile Mousso Africa, Ivorian woman, Embargo, Betty De Asta, Evelyne, Loketo na kadhalika.

Tarehe 19 Machi 2020 taarifa kutoka Paris, Ufaransa, zilitolewa kwamba Aurlus Mabele amefariki kwa ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya albamu zake:

 • Dossiwer X 2000 (JPS Production)
 • Compil two 1999 (DEBS Music)
 • Compil one 1999 (DEBS Music)
 • Tour de contrôle 1998 (JPS Production)
 • Best of Aurlus Mabele 1997 (Mélodie) CD 41044 2
 • Album 1997 1997 (Mélodie)
 • Album 1996 1996 (Mélodie) CD 41041 2
 • Génération-Wachiwa encaisse tout 1994 (JIP) CD 41032 2
 • Stop Arretez ! 1992 (JIP) CD 41021 2
 • Embargo 1990 (Mélodie)
 • Soukouss la terreur 1989 (Mélodie) CD 41007-2
 • Sebene
 • Africa Mousso (Femme D'Afrique)
 • La Femme ivoirienne
 • Maracas d'or 1988
 • Loketo : réconciliation/cicatrice
 • Loketo:Confirmation

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aurlus Mabele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.