Augusto wa Bourges
Mandhari

Augusto wa Bourges (alifariki Bourges, Ufaransa, 560 hivi) alikuwa mlemavu wa mikono na miguu asiyeweza kutembea ila kwa kutumia magoti na viwiko. Alitumia sadaka alizopewa kujenga kanisa kwa heshima ya Mt. Martino.
Alipomaliza tu, alipona kikamilifu ulemavu wake akakusanya wamonaki akawa padri na abati akidumu katika sala [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |